tiko
tiko
IGENGA MTATIRO, TARIME
MKAZI wa
Kitongoji cha Nyaiheta, Kijiji cha Kewanja Kata ya Kemambo wilayani
Tarime, Mara, Marwa Omtima (55) ambaye ni kada wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), ameuawa kwa kupigwa mshale tumboni na mtu
aliyetajwa kwa jina la Gamaina, mkazi wa kitongoji hicho kulipotokea
ugomvi usiku wa Machi 5, mwaka huu.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime
na Rorya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema siku ya tukio,
marehemu alipigwa mshale majira ya usiku na kufariki dunia.
Jeshi hilo lilisema linaendelea kumsaka
mtu aliyefanya mauaji hayo ili kumkamata na kumfikisha mahakamani kujibu
tuhuma zake za kuua huku chanzo kilidaiwa ni ugomvi binafsi uliotokana
na chuki za siku zilizopita.
Ilielezwa kuwa, marehemu alifariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya
kuvuja damu nyingi.Katika mazishi yaliyofanyika Machi 7, mwaka huu,
msemaji wa familia hiyo ambaye ni kaka wa marehemu Omtima, Masanda
Omtima, aliwaambia waombolezaji kuwa, familia haitakuwa na kisasi na
familia ya mtuhumiwa.
Aliwaomba wanafamilia wa pande zote
kuendelea kutembeleana kama zamani huku akisema ni dhambi kuua mtu kwani
aliye na mamlaka ya kuondoa uhai wa binadamu ni Mungu.Kutokana na tukio
hilo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyamwaga aliyehudhuria mazishi hayo, OCD
Simon Marwa Maigwa alisema atahakikisha muuaji huyo anasakwa mahali
popote alipokimbilia na kutiwa nguvuni.
Miongoni mwa waombelezaji wa msiba huo
walioshindwa kutoa ujumbe wao kwa simanzi ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa
wa Mara, Esther Nicholas Matiko aliyesema tukio hilo limetia aibu na
kuichafua Mara.
Mazishi hayo yaliyovuta hisia za watu
wengi kutoka vyama vya siasa na viongozi wake, jamii na askari polisi
kwani aliyeuawa kaka yake ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja Tanzania,
Omtima (Chadema).
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment