tiko
tiko
BABA mzazi wa staa wa filamu za Kibongo,
Rose Ndauka, Donatus Ndauka anadaiwa kumtaka mwanaye huyo kuangalia
uwezekano wa kuingia maisha ya ndoa kwa vile siku zinakatika kama mvua
za masika.
Kwa mujibu wa chanzo, baba huyo mwenye
makazi yake jijini Tanga alimpigia simu mwanaye mapema wiki hii baada ya
kusoma habari kupitia Magazeti ya Global ikimkariri mzazi mwenzake na
staa huyo, Malick Bandawe akisema hakuna mwanamke kama Rose.
Malick alisema licha ya kumwagana na
Rose mwaka jana, lakini bado anamkumbuka na kumthamini kama mzazi
mwenzake kwa vile ndiye anabeba jukumu la kumwangalia mtoto wao, katika
maisha ya kila siku.
“Baba yake alimwambia Rose kama kuna
mwanaume anayesema anampenda kwa sasa basi amuoe na si kupoteza muda
kwani siku zinakwenda sana. “Pia baba yake alimwambia anajua aliachana
na Malick lakini kama ataona kuna mawazo yanamshauri kujenga upya
uhusiano wao uliobakiza ndoa tu, aangalie mwenyewe Rose kwa vile ni mtu
mzima sasa, ila asichopenda baba yake ni kusikia leo huku, kesho kule,”
kilisema chanzo hicho.
Amani lilimtafuta Rose kwa njia ya simu
ambapo lilipomuuliza kama kweli alipewa ujumbe huo na baba yake alisema:
“Iwe kweli au si kweli, kuna mambo ya familia, pia kuna mambo ya
jumuiya.
Sasa kama kweli niliambiwa hivyo na baba yangu unataka na wewe nikwambie ili iweje?”
Amani: “Wewe ni staa bwana, lolote kwetu ni habari.”
Rose: (akakata simu).
Amani: “Wewe ni staa bwana, lolote kwetu ni habari.”
Rose: (akakata simu).
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment