tiko
tiko
BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala
Masanja kudaiwa kumuibia bwana aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu
kwa muda mrefu na kukosa ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi
wa SMS za mapenzi za Kajala na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo
zimenaswa, Amani linakumegea mchongo kamili.
Chanzo makini kilichokuwa karibu na
Kajala na kigogo huyo, kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa
meseji za Kajala kupitia kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu
katika penzi na Wema kisha kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.
“Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi
nikafanikiwa kupata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema, kama vipi
niwatumie,” kilisema chanzo chetu.Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho
kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa
akiitana baby na kigogo huyo, huku wakiwa ‘dip kimalovee’ kiasi cha
kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala mahitaji mbalimbali.
“Jamaa walikuwa wanapika na kupakua,
kigogo alikuwa akigharamia kila kitu, kuanzia misosi ya nyumbani,
usafiri wa location na hata kwa wazazi wa Kajala, alikuwa anatuma
fedha,” kilisema chanzo hicho.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuzinasa
SMS hizo na kujionea zikiwa na majibizano ya muda mrefu huku zikitaja
pia marafiki wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.
Baada ya paparazi wetu kumwagiwa SMS
hizo, alimvutia waya Kajala ambaye alizikana SMS hizo na kuomba atumiwe
ndipo atoe jibu ambapo mwandishi wetu alifanya hivyo lakini hakujibu
chochote na hata alipopigiwa tena, hakupokea.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment