tiko
tiko
Picha / Habari: Johnson James, GPL / Mwanza
Watu watano katika Wilaya ya Nyamagana
jijini hapa wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na kifusi wakati
wakiwa kwenye maandalizi ya kujenga jengo lililotegemewa kuwa na ghorofa
saba, eneo la Nyerere Road, leo majira ya saa sita mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo
la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Kunisaga amesema kuwa
amesikitishwa na tukio hilo ambapo watu hao wameangukiwa na ukuta wakati
wakijenga msingi wa jengo hilo na hii ni kutokana na kuwa na
wakandarasi ambao hawajengi majengo kwa kiwango kinachotakiwa.
Katika hatua nyingine, Kunisaga amesema
kuwa hali ya Watanzania kuwa wanapoteza uhai wao kila kukicha kutokana
na kuangukiwa na vifusi, serikali haiwezi kukubaliana nayo hivyo
amesitisha ujenzi wa jengo hilo.
Majeruhi waliokumbwa na tukio hilo
wameongea na waandishi wa habari japo kwa taabu na kusema kuwa ukuta
uliowaangukia ulikuwa umeunganishwa kama uzio hivyo wakati wakiendelea
kuchimba msingi, uzio huo ulikuwa ukiendelea kutitia hivyo kusababisha
kuporomoka na kuwaangukia.
Daktari wa zamu wodi ya dharura, Ernest
Elisenguo amethibitisha kupokea majeruhi watano ambao wametokana na
tukio la kuporomokewa na kifusi na kuwataja kuwa ni Ramadhan Hussein
Nyarandu, Rashid Mkumba Hamis, Elias Bahati, Benson Agustino na Mtani
ambapo watatu kati ya hao hali yao imeendelea vizuri na wameruhusiwa
kwenda nyumbani ila wawili kati yao bado hali zao siyo nzuri na
wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Majeruhi Rashid Mkumba Hamis, ameeleza
kama ifuatavyo: "Mimi ni fundi na nilikuwa natengeneza 'bezi' kwa ajili
ya kushikilia nguzo za ghorofa wakati ninaendelea na kazi yangu
nikaanza kusikia udongo ukiniangukia mgongoni, ghafla nikasikia matofali
yananiangukia.
Katika kujiokoa matofali yakawa
yameniangukia kwenye miguu na bahati mbaya kwa mujibu wa madaktari ni
mwamba nimevunjika mguu ila namshukuru mungu kuona niko salama."
tiko
tiko
Post a Comment