tiko
tiko
Akiongea na East
Africa Radio kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mbeya ACP, Ahmed
Msangi amesema vurugu hizo zimetokana na mgogoro wa kiwanja baina ya
chama cha Mapinduzi CCM na wananchi ambao wamekuwa waking'ang'ania
kumiliki kiwanja hicho licha ya maamuzi ya mahakama kutaja CCM ndio
mmiliki halali wa kiwanja hicho.
Amesema vurugu
hizo ambazo zimesimamisha shughuli zote biashara na kukwamisha pia
usafiri katika barabara kuu ya Tunduma, zilianza siku ya jumatatu baada
ya wananchi kuhamasishwa na kuvamia uwanja huo na kuanza shughuli za
ujenzi wa Zahanati pamoja na Kituo cha polisi, ambapo polisi waliingilia
kati na kuwazuia.
Kamanda Msangi
amesema watu 26 walikamatwa siku ya Jumatatu katika vurugu hizo ambazo
zilisambaa katika barabara kuu na kusababisha barabara kufungwa kwa
kuwekwa mawe ambapo pia gari moja la polisi lilivunjwa vioo
Amesema baada ya
jana hali kutulia kidogo leo tena vurugu hizo ziliibuka baada ya
wananchi kukutana na mbunge wa eneo hilo kupitia Chadema Mhe. David
Silinde ambapo wananchi walirejea tena kufanya vurugu mitaani na kufunga
barabara kwa mawe na kuchomamoto matairi ya gari, hata hivyo polisi
walituliza hali hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment