tiko
tiko
MAMBO mengine ni ya kuyasikia
yakiwatokea wenzako na usiombe yakakukuta kama ilivyomtokea msichana
huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja baada ya kuchukua kipigo
‘hevi’ ambacho nusura apoteze maisha yake, maeneo ya Sinza Afrikasana,
juzi Jumatatu.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema, binti
huyo akiwa na mwanaume mmoja, walionekana wakitoka katika baa iitwayo
Kona, wakiongozana hadi kwenye baa nyingine iliyo maeneo ya Afrikasana
ambako waliendelea na kinywaji.
“Yule msichana ni mmoja wa wanaojiuza
pale Kona, nadhani walikuwa na makubaliano ambayo wamefikia, maana
walikuwa wakinywa kwa raha zao, ghafla tukasikia wanaanza kuzozana,
jamaa alikuwa anataka waondoke, bibie akawa analeta longolongo,” alisema
dada mmoja aliyekuwa eneo la tukio.
Inadaiwa kuwa dada huyo alianza kupiga
yowe akitaka apewe kiasi cha shilingi 30,000, ndipo mwanaume huyo ambaye
alitoweka haraka, alipoamua kumpa kipigo kikali kiasi cha kumpasua
kichwani na kumsababishia maumivu makali.
Baada ya kupokea kipigo hicho, baadhi ya
wahuni walifika eneo hilo na kuendelea kumfanyia vitendo vya
kidhalilishaji hadi akina mama wa eneo hilo walipoamua kumhifadhi kwa
kumfunika kanga, lakini katika hali ya kushangaza, msichana huyo
alipitiwa na usingizi mzito.Kuona hivyo, majirani hao waliamua kumpeleka
polisi ambako hata hivyo alifukuzwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni
mlevi.
tiko
tiko
Post a Comment