tiko
tiko
DAKTARI mmoja
bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na
nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni mgonjwa
aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa utoto
wake.
Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya
kuombwa kuzungumzia tabia za Shilole za kugombana mara kwa mara na
mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia
linalomsumbua mmoja wao au ni ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.
“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa
unyanyasaji akiwa mtoto ‘child abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa,
kupigwa, kunyimwa chakula au mateso ya aina hiyo, akikua bila kupata
tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu
mzima.
“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na
kupenda kujitenga, hasira za karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni
kumfanyia mtu mwingine hasa mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu
wanaita ‘Propensity Victimization,’” alisema daktari huyo.
Alisema katika nchi zilizoendelea,
tatizo hilo hupewa kipaumbele katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi
nyingi za kiafrika kwani madhara yake huwa ni pamoja na mwathirika
kuamua kujinyonga au kuua.
Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana
kufanana na matukio yaliyowahi kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa
miaka 14, aliwahi kubakwa, pia anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu
wenye umri mkubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri
mdogo.
tiko
tiko
Post a Comment