tiko
tiko
Picha ya juu hapo ni shuhuda akisimulia namna alivyokerwa na ukatili aliyofanyiwa mwanamke mwenzie huko Tabora.
Vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya akinamama imebainishwa kuwa ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa wilayani urambo mkoani tabora ambapo, mwanamke mmoja amefanyiwa ukatili, wa kipigo na kuwekewa mti katika sehemu zake za siri, kisa kikiwa ni wivu wa kimapenzi.

Akizungumza
nyumbani kwa mama huyo mtendaji wa kata ya urambo Bw. Ezekiel Marwa
amesema kuwa, ukatili aliofanyiwa mama huyo ni wa kinyama, kutokana na
kupigwa sana kichwani,hali ambayo mama huyo amepoteza kumbukumbu, pamoja
na uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali.
Aidha
Bw. Ezekiel amesema kuwa, katika hali ya kushangaza ambapo baadhi ya
wanandugu walitaka kufifisha kesi hiyo kwa kumtafuta mganga wa kienyeji,
ambaye alidaiwa angetengeneza dawa ili pasiwepo na kesi, lakini mganga
huyo wa jadi, katika nyumba hiyo alimfanyia ukatili wa ubakaji
mwanafunzi wa darasa la sita.
Baadhi
ya wananchi ambao siku ya tukio walikerwa na kitendo hicho ambao
walitaka kumuua mshambuliaji huyo wamesema kuwa, unyanyasaji kama huo
usifumbiwe macho na serikali bali kutoa adhabu kali kutokana na kupoteza
mwelekeo wa maisha kwa mama huyo ambaye amekuwa tegemezi.
Akizungumza
kwa njia ya simu kaimu kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina
msaidizi Juma Bwire amebainisha tukio hilo akidai watuhumiwa wamepelekwa
mahakamani.
Picha hapa juu ni mwanamke aliyefanyiwa ukatili akiwa kafichwa sura wakati akieleza namna ilivyokuwa.
tiko
tiko
Post a Comment