tiko
tiko
Wakati
wenyeviti wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
pamoja na kamati zake za kitaalamu wanakutana Zanzibar kutafuta suluhu
kuhusu mgawanyo nafasi za kugombea katika uchaguzi mkuu ujao, kuna
uwezekano mkubwa vyama hivyo kuteua mgombea urais kutoka Chadema.
Tovuti hii inaweza kuripoti kwa uhakika
kuwa uwezekano huo unatokana na vigezo vinavyotumiwa na vyama hivyo
kusimamisha mgombea mmoja kwa kila jimbo na kwenye nafasi ya urais
ambavyo vinaipa Chadema nafasi hiyo dhidi ya vyama vingine katika umoja
huo ambavyo ni CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
Vigezo hivyo ni matokeo ya uchaguzi
2010, idadi ya madiwani kwa kila chama, matokeo ya uchaguzi wa Serikali
za Mitaa wa Desemba mwaka jana, mtandao wa chama nchini na nguvu ya
mgombea iwapo Chadema kitamsimamisha katibu mkuu wake, Dk Willibrod Slaa
kwa mara ya pili.
Taarifa zilizolifikia Mwananchi kutoka
ndani ya kamati ya ufundi ya Ukawa zinasema pamoja na kuwapo mvutano
katika baadhi majimbo Tanzania Bara, kwa upande wa Zanzibar hakuna
tatizo hilo, jambo linaloipa CUF nafasi ya moja kwa moja kwenye ubunge,
uwakilishi na hata urais wa visiwa hivyo.
Kwa mujibu wa habari hizo, nafasi nzuri
ya CUF kupita moja kwa moja Zanzibar bila ushindani ndani ya Ukawa,
inatoa fursa kwa upande wa Bara, kwa vyama vilivyosalia kupitishwa
kuwania urais wa Muungano.
Hata hivyo, kwa vigezo vilivyotajwa hapo
juu, Chadema ndiyo inakuwa na nafasi isiyo na kipingamizi kutokana na
rekodi vyama vilivyosalia Bara.
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Chadema
kilimsimamisha Dk Slaa na aliibuka wa pili baada ya Rais Jakaya Kikwete
akiwa na kura 2,271,941 (asilimia 26.34) akifuatiwa na Profesa Ibrahim
Lipumba aliyepata kura 695,667 (asilimia 8.06) na Hashim Rungwe wa
NCCR-Mageuzi aliyepata kura 26,388 (asilimia 0.31). NLD haikusimamisha
mgombea urais.
Kwa upande wa majimbo yaliyotokana na
uchaguzi wa 2010, Chadema kiliongoza kikiwa na wabunge 24 (wote kutoka
Bara), CUF 23 (wawili kutoka Bara, 21 Zanzibar) na NCCR-Mageuzi wanne
(wote wa Bara).
Katika rekodi za uchaguzi wa mitaa
zilitolewa na Tamisemi kabla ya chaguzi za marudio, Chadema ilipata
mitaa 980, ikifuatiwa na CUF (mitaa 266), NCCR Mageuzi (28) na NLD
mtaa mmoja. Kwa upande wa vijiji, Chadema kilishinda vijiji 1,754, CUF
(516), NCCR-Mageuzi (67) na NLD vijiji viwili.
Hata kwa upande wa vitongoji Chadema
kiliviongoza vyama hivyo kwa kupata vijiji 9,145 kikifuatiwa na CUF
(2,561), NCCR-Mageuzi (339) na NLD vitongoji viwili.
Tayari NCCR-Mageuzi kimeonyesha nia ya
kumteua Dk George Kahangwa kuwania urais wakati Mwenyekiti wa NLD, Dk
Emmanuel Makaidi alikaririwa na gazeti hili hivi karibuni akisema kuwa
chama chake kimekwishamteua kuwania urais, hivyo jina lake litapelekwa
Ukawa kushindanishwa.
tiko
tiko
Post a Comment