tiko
tiko
Taasisi
ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji
ambao inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali
itashindwa kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini
ya kiislam popote walipo kuipigia kura yaHapana Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Kauli
ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa
na muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki
(TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Baraza la Makanisa la
kipentekoste(CPCT) ambao wote kwa pamoja waliwataka waumini wa dini ya
kikristo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa kutokana na serikali kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
Akitoa
tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam ambalo ni muunganiko wa taasisi za
dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati
wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya habari jana Jijini Dar es Salaam,
aliitaka serikali kuwachukulia hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya
uchochezi.
“Serikali
iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko
yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume
cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
Aidha,
Sheikh Katimba aliitaka Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji
mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya
sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu mawili.
Mosi: Serikali iache njama na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.
“Endapo
serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi
unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika
kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali
haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi” alisema Sheikh Katimba.
Pili: Serikali
igharamie mahakama hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri
yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo
mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
“Na
pia mahakama hiyo igharamiwe na serikali kama inavyogaramia huduma za
makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding
(MOU) , mkataba ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema sheikh huyo
tiko
tiko
Post a Comment