tiko
tiko
Staa wa muziki wa mduara, Snura Mushi
ameingia katika tuhuma nzito akidaiwa kutoka kimapenzi na mume wa rafiki
yake Halima Yahya ‘Davina’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, kwa
kipindi kirefu, Snura amekuwa akionekana nyakati za usiku akiwa na mume
wa Davina, wakati mwingine mwanaume huyo anaenda nyumbani kwa Snura au
wawili hao kuzungumza kwa muda mrefu ndani ya gari la mwanaume huyo.
“Yaani mastaa wa Bongo bwana, wanapenda
sana kuchukuliana mabwana. Huyu Snura anatoka na mume wa mwenzake. Mume
wa Davina huwa anakuja nyumbani kwa Snura mara kwa mara hasa nyakati za
usiku.
“Wakati mwingine anakuja na gari na
kupaki jirani na nyumbani kwa Snura kisha wanakaa kwenye gari kwa saa
kibao. Snura anamzunguka rafiki yake, fuatilieni mtaujua ukweli,”
kilisema chanzo chetu.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa
Wikienda liliamua kuingia mzigoni kwa kumsaka Snura na alipopatikana,
akasomewa tuhuma zake ambapo katika hali ya kushangaza, msanii huyo,
alimwaga chozi.
Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’.
Alipomaliza kulia, Snura alianza
kufunguka ukweli wa kisa hicho ambapo alikiri kuwa ni kweli mume wa
Davina alikuwa akienda nyumbani kwake mara kwa mara lakini ilikuwa ni
kipindi ambacho Davina na mwanaume huyo walikuwa wametibuana kiasi cha
msanii huyo kufungasha virago vyake na kutokomea kusikojulikana.
“Mimi nilikuwa nahangaika kuwapatanisha
kwa sababu walikuwa kwenye mgogoro mkubwa, mumewe akawa ananiomba
nimsaidie kumbembeleza Davina arudi wayazungumze na kumaliza matatizo
yao ili kuokoa ndoa yao isivunjike.
Ijumaa Wikienda halikuishia hapo,
lilimtafuta pia Davina ili kujua kwa upande wake analizungumziaje sakata
hilo ambapo msanii huyo alitema nyongo. Hebu msikie:
“Watu wengine hawana kabisa kazi za
kufanya, yaani walikuwa wanataka kunigombanisha na shosti wangu lakini
wameshindwa. Ni kweli na mimi niliwahi kuletewa taarifa kwamba mume
wangu anaonekana nyumbani kwa Snura usiku lakini ilikuwa ni kipindi
ambacho nilikuwa kwenye matatizo na mume wangu.
“Kiukweli Snura hawezi kufanya hivyo kwa
sababu yeye ndiye aliyepigania ndoa yangu isivunjike. Isitoshe sisi
tunaishi kama ndugu, watoto wangu huwa wanaenda kushinda kwake na wakati
mwingine huwa namtuma mume wangu akawachukue kwa hiyo hata kama
wanamuona kwake, siyo kwa nia mbaya, watu aache uchonganishi,” alisema
Davina.
tiko
tiko
Post a Comment