tiko
tiko
Halafu kilichokuwa kinanipa wivu zaidi ni kuwa hawa rafiki zangu wengi
tumetoka kijiji kimoja, nawajua mpaka wazazi wao, na najua kwenye ukoo
wao hakuna anayejua Kingleza kabisaaa.
Kimoyomoyo nikawa najisemea nikipata mtoto lazima na mimi nihakikishe
anajua Kingleza bado mdogo, kuwaringishia ndugu zangu. Hasa kuna kakangu
flani anaringia sana hela zake, ingekuwa Jumapili asubuhi najidai
namtembelea halafu nakaachia katoto kangu kawe kanaongea Kizungu mbele
yake, hiyo lazima ingemchanganya maana hajui hata neno moja la Kizungu,
hahaha, we ngoja tu.
Mungu si Masanja, mke wangu akazaa katoto ka kike, kila siku nikawa nakangoja kakue kaanze nasari.
Nikaulizia kwa jamaa nasari gani inafundisha vizuri kingleza, nikaambiwa Fudenge Intaneshno Nasari Skul, ni kiboko, mwenyewe nikaenda kuiona kwa kweli nilifurahi, mabembea, walimu wanaongea Kingleza tu, vyoo visafi vina malumalu, vitabu vyenye picha za watoto wa Kizungu, yaani kila kitu kama Ulaya.
Nikaulizia kwa jamaa nasari gani inafundisha vizuri kingleza, nikaambiwa Fudenge Intaneshno Nasari Skul, ni kiboko, mwenyewe nikaenda kuiona kwa kweli nilifurahi, mabembea, walimu wanaongea Kingleza tu, vyoo visafi vina malumalu, vitabu vyenye picha za watoto wa Kizungu, yaani kila kitu kama Ulaya.
Hatimae mwanangu akaanza shule. Ada ya mwezi ilikuwa kubwa kuliko kipato
changu cha mwezi, lakini ilikuwa lazima nistrago ili na mtoto wangu
ajue Kingleza. Wala haikupita wiki mtoto akaanza kuongea kimombo na
kuanza kutuchanganya mimi na mama yake maana tukawa mara nyingi
hatumuelewi, tunaishia kusema ‘Yes’ kila akisema neno la kingleza.
Yaani hata kulia mtoto akawa analia Kizungu, ‘No mother no, giv ais krim
hata sijui alikuwa anataka nini , basi atalia hapo mpaka labda tumpe
biskuti au soda ndiyo ananyamaza. Walimu walituletea barua inayoelekeza
vyakula muhimu kwa mtoto, vyote vya Kizungu, milk, juice, hamburger,
sausages, na eggs hivyo lazima mtoto ale kwa makuzi mazuri ya Kizungu,
na mtoto alikuwa analia sana akiamka na kukuta chai kwa maandazi
asubuhi.
Pamoja na joto la jiji letu hili la Dar es Salaam niliambiwa nimnunulie
sweta ambazo zinauzwa shuleni kwa laki mbili na tai mbili za kubadili
kila wiki, pia atafutiwe begi la mgongoni la kubebea vitabu, tena siyo
mtumba linatakiwa litoke dukani, kuna duka la watoto wa wenye hela na
mabegi yanauzwa hapo, na sisi tukaelekezwa huko.
Kiukweli hela yote niliyokuwa napata huku na kule iliishia kwenye
matumizi ya shule ya mtoto. Kingleza kilikuwa kinaongezeka kila siku,
hata akicheza na watoto wenzie yeye ni Kingleza tu, kimoyomoyo nilikuwa
najisifu sana kwa kweli.
Hatimae tukaambiwa tunakaribishwa kwenye siku ya wazazi, nikaazima suti
na mke wangu akavaa bonge la kitenge na kofia kubwa kama ya mama
mchungaji, tukaenda shule, kwenye siku ya wazazi.
Tukaonyeshwa pa kukaa shamra shamra zikaanza, kama kawaida ya kwetu
hotuba ndefu zikatolewa na Mkurugenzi wa nasari, mwalimu mkuu wa nasari,
mwalimu wa darasa la nasari, muwakilishi wa wazazi wa nasari, hatimae
mgeni wa heshima ambaye najua watoto walikuwa hawana hata habari naye
akaongea nao na kuwaasa wasome waje kuwa viongozi wa kesho.
Yakaanza maonyesho ya watoto, watoto wakawa wanatoka mmoja mmoja na kuonyesha jinsi wanavyojua Kingleza.
Hatimae tukaambiwa watoto sasa watakuja kucheza ngoma ya kiasili. Si
ndiyo vitoto vyote vikaja mbele yetu kiunoni vimejifunga kanga, Dj
akaanzisha wimbo wa Kinaijeria ‘Chop my mani, chop my mani’ vitoto
vikaanza kukatika kiuno, mzazi mmoja akainuka kumtunza mwanae na mimi
nikaenda kumtuza wangu. Kwa kweli hii shule kiboko inafundisha Kiingleza
kila kitu mpaka ngoma za kiasili wanacheza nyimbo za Kiingleza
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment