tiko
tiko
Ukitaka kujua hali yangu, mimi niko poa na ninaendelea na majukumu yangu
ya kujenga taifa kama kawaida na barua hii ni sehemu ya majukumu yangu
ya kazi hivyo lazima nikuandikie tu, sina jinsi.
Dhumuni la barua hii kwanza kabisa ni kutaka kukukumbusha kidogo umuhimu wako katika jamii. Sitaki kuamini kwamba hujui umuhimu wako lakini kukumbushana ni muhimu, binadamu tumeumbwa kusahau.
Dhumuni la barua hii kwanza kabisa ni kutaka kukukumbusha kidogo umuhimu wako katika jamii. Sitaki kuamini kwamba hujui umuhimu wako lakini kukumbushana ni muhimu, binadamu tumeumbwa kusahau.
Chid wewe ni mwakilishi mzuri sana wa Muziki wa Hip Hop. Tangu kipindi
kile ulichosumbua na wimbo wako wa Dar es Salam Stand Up na nyingine
kibao.Ulikuwa hukosei, ulikuwa unaachia jiwe baada ya jiwe na kila mtu
alikuwa anakubali uwezo wako.
Kudhihirisha wewe ni mkali, nakumbuka ulikuwa ni lulu katika suala zima
la kolabo. Wasanii walikuwa wakipanga msururu kukusaka, waliamini
ukiingiza sauti yako katika nyimbo zao basi nazo zitakuwa tamu kama
mcharo.
Hilo halikuwa na kificho, ulifanya kolabo nyingi sana. Nyimbo kama Neila
ya Tunda Man, Hao na nyingine kibao zilinoga sana pale ulipoingiza
sauti yako yenye mamlaka ambayo ulijua kuipangilia na kuendana na biti,
wewe ni mkali aisee!
Pamoja na uzuri huo, juzikati hapa liliingia suala la wewe kunaswa na
madawa ya kulevya. Binafsi sikushtuka sababu dalili za wewe kutumia
nilishaziona kabla.Niliona dalili kutokana na matendo yako, yalikuwa
hayafanani na uwezo wako mkubwa wa kutunga mashairi yenye uzito. Matukio
kama yale ya kumdunda msanii mwenzako, Rehema Chalamila ‘Ray C’,
nilijua kabisa si wewe.
Lilipokuja kutokea lile la kukamatwa na madawa pale Air Port,
nilisikitika sana kama shabiki wako. Suala la wewe kuanza kuingizwa
kwenye mikono ya sheria ni kuzidi kudidimiza kipaji chako na muziki wako
kwa jumla.
Nilifuatilia kwa makini kesi yako hadi pale ulipotakiwa kulipa faini
nikasema ni jambo la heri lakini unapaswa sasa kubadilika kweli na
kutokubali kurudi nyuma. Uliwahi kukiri kuwa unatumia madawa, ukaahidi
kuacha lakini ukarudia.
Nikushauri, mimi pamoja na mashabiki wengi Bongo na nje tunakupenda na
tunahitaji kuendelea kusikia ‘madini’ yako.Ngoma yako ya Kimbiza ambayo
haina muda mrefu sana tangu uiachie inatosha kuonesha kwamba uwezo unao,
tupe raha kama ile ambayo ulikuwa unatupa.
Achana kabisa na madawa ya kulevya, sitegemei kukuona tena unakamatwa au
unahusishwa katika suala hilo kwa namna yoyote.Ni matumaini yangu
utabadilika kweli, kwa leo ni hayo, kila la kheri!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment