tiko
tiko
Jamani kuna mambo mengine yanasikitisha, hivi kwa nini umuogope mwanamke
mwenzio mwenye viungo kama wewe. Wiki iliyopita nilielezea makosa ya
nyuki kukimbia mzinga wake kwa sababu tu mtu katia mkono na kulamba
asali yake.
Jamani ukiona mtu katia mkono kwenye mzinga wako ujue asali yako tamu,
unatakiwa kuilinda na siyo kuukimbia mzinga ili kuwaruhusu watu
wajilambie kwa raha zao, haipendezi. Hizo ni hasira za mkizi na kutoa
kafara kwa mvuvi. Nimeliongelea hili kwa vile makavu ya leo yanafanana
na hilo.
Juzi nilikutana na mtoto wa shoga yangu akiwa anatoka sokoni, katika
mazungumzo yetu si unajua mimi mtu wa utani. Sijui kukasirika kijinga,
mtoto wa kike niliumbwa siku Mungu akitabasamu, nami nikawa na umbile la
tabasamu siyo wewe uliumbwa Mungu amechoka kila wakati uso kama ndimu,
unacheka hujulikani, umenuna hujulikani!
Si kwanza nazungumza wenye sura mbaya bali wenye sura zilizokosa
tabasamu, siwezi kumhukumu mtu kwa maumbile kwa vile mimi sijawahi
kuumba wangu. Ila nazungumza na tabia za watu, Mungu kawaumba na sura
nzuri lakini imeharibika kwa kukunja uso na kupinda midomo!
Hebu tuachane na hayo tuendelee na yetu, basi katika kutaniana si ndiyo
aliponieleza kaamua kurudi kwao baada ya mumewe kuoa mwanamke mwingine.
Nilimuuliza kipi kikubwa kilichomuondoa kwa mumewe ikiwa dini yake
inamruhusu. Alinijibu jibu la kitoto ambalo lipo katika vichwa vya
wanawake wengi!
Eti ameondoka kwa vile hawezi kushea mwanaume na mwanamke mwenzake. Jibu
lake nililinifanya nimwangalie chini mpaka juu mpaka akashtuka na
kuniuliza kulikoni kumuangalia vile. Nilichomueleza nataka na wewe ukae
chini nikueleze uache ujinga!
Jamani ni kweli wanawake tupo kama mdudu wa sikio tusiotaka mshirika,
lakini kutokana na hali ya sasa hivi kuwa na wako wa peke yako kazi.
Afadhali dini zingine zinaruhusu mpaka wake wanne, lakini dini
zilizokataa tunaona jinsi gani viongozi wao wanavyoingia kwenye kashfa
ya kuwa na wanawake wengi tofauti na muongozo wao.
Siyo kwamba nahalalisha lakini ukweli ndiyo ulivyo, asilimia kubwa ya
nyumba zetu waume zetu wana wanawake zaidi ya mmoja. Wengine
tunawakamata na wasichana wetu wa kazi imefikia hata kuwapa ujauzito!
Hii yote inatokana pengine na udhaifu wetu ndani ya ndoa kwani wengi
baada ya kuolewa hujisahau na kuamini ukiishaolewa ndiyo kila
kitu.Tumekuwa hatuzithamini ndoa zetu kwa kuamini baada ya kuolewa
hakuna kingine zaidi kwa mumeo kama umemvulia nguo ya ndani ndiyo
baaasi. Tunasahau mwanaume unatakiwa kutunzwa kama mtoto, kwani wewe
ndiye kila kitu kwake siyo kasoro zitolewe na mwanamke wa pembeni.
Pengine mumeo hakuwa na wazo la kuongeza mwanamke mwingine, lakini
mwanamke mwenzako ameyaona mapungufu yako na kuyafanyia kazi ndiyo
yaliyomfanya mumeo aingie kichwakichwa baada ya kunasa, aliendelea kumpa
vitu adimu ambavyo kwako hapati. Ili afaidi vizuri anamuoa kabisa ili
asile kwa kujificha.
Unaletewa mke mwenza unakimbia kumbe sababu ni wewe. Kaingia ndani
hutakiwi kukimbia, jirekebishe, pigana kuhakikisha unairudisha namba
moja yako.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment