tiko
tiko
Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota hivi karibuni alipoteza fahamu
baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi
wake, Gharibu Dumba.
Tukio hilo lilitokea kwenye Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es
Salaam ambapo alikwenda bila kujua kuwa mtu wake huyo alikuwa na jambo
kubwa la kumfanyia.
Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile, alishangaa akivishwa
pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo gharama yake ni takriban
shilingi milioni 3.
Akizungumzia tukio hilo mtangazaji huyo alisema: “Nilipata mshituko
kwani sikutarajia na ndiyo maana nikapatwa na hali ile. Namshukuru Mungu
kwa hili lililonitokea, ni jambo la heri na Mungu aniongoze katika
safari hii ya kuelekea kwenye maisha ya ndoa.”
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment