tiko
tiko
Baada ya kufanya msako katika nyumba yake. Polisi
nchini Ujerumani wamegundua kile wanachosema kitawasaidia katika
kubaini kiini cha rubani msaidizi Andreas Lubitz, kuangusha ndege na
kuwauwa abiria wote 150.
Polisi hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana
na kile walichokipata, lakini baadhi ya vitu vyake vikiwemo Kompyuta,
vimechukuliwa ili kuchunguzwa.
Huku uchunguzi huo ukiendelea,
imebainika kuwa rubani huyo alitatiza kwa muda, mafunzo yake ya urubani
mwaka 2008, kutokana na kutibiwa matatizo ya kiakili.
Waziri wa maswala ya ndani nchini
Ujerumani, Tomas de Maiziere, anasema kuwa, uchunguzi wa kiusalama dhidi
ya rubani huyo, haujasema lolote huku, muajiri wake kampuni ya
Lufthansa, ikisizitiza kuwa Lubitz alikuwa asilimia mia kuendesha ndege.
NA BBC SWAHILI
tiko
tiko
Post a Comment