tiko
tiko
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,limemtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Hatua
hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko, ambapo
inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya Kardinali
Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba Inayopendekezwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.
Kova alisema jeshi hilo limepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Kardinali Pengo.
Alisema matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.
Kova alisema baada ya tukio hilo, juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kumpata Mchungaji Gwajima bila mafanikio.
“Ni muhimu sana kwa Mchungaji Josephat Gwajima aripoti mwenyewe badala ya kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.
“Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Kamanda Kova.

VIDEO YA GWAJIMA
Hivi karibuni
sauti iliyorekodiwa na picha za video zilionekana katika mitandao ya
kijamii ambazo zilikuwa zikimtukana Kardinali Pengo.
Sehemu ya maneno hayo ambayo yanamwonyesha Gwajima akizungumza kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Facebook ni; “Pengo unaaibisha kama mtoto mdogo aliyevaa pampasi aliyebebwa na mama yake, Pengo ni mjinga asiyefaa, juzi aliokoka kwa kula chakula chake ovyo ovyo, sijui kala maharage ya wapi?
“Pengo awe Mkatoliki amejishushia heshima yake mwenyewe, aache uaskofu awe mkulima wa kawaida, hafai mzee ametudhalilisha kabisa na amewageuka maaskofu wote kwa kile walichopatana .
“Amewadhalilisha maaskofu wote, amedhalilisha CCT, amedhalilisha CPCT, pia amewadhalilisha Watanzania wote.”

GWAJIMA NI NANI
Gwajima ni
mwasisi na mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambapo kwa sasa
anaongoza waumini wapatao 70,000 kwa siku, na hivi sasa yuko mbioni
kuanzisha makanisa mengine mikoa yote ya Tanzania.
Kwa mujibu wa kauli zake alizopata kuzisema huko nyuma katika moja ya mahubiri yake kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kawe jijini Dar es Salaam, hivi sasa ana waumini wengi kuliko makanisa mengine kutokana na huduma nzuri anayotoa kwa waumini na jamii kwa jumla.
“Nimefanikiwa kuwa na waumini wengi kuliko wengine kwa sababu nahubiri Neno tu, sirushiani maneno na makanisa mengine.
“Sisi hatuna utamaduni wa kuwashambulia wachungaji wenzetu. Wao hata wakitusema vipi, sisi tunakaa kimya kwani kujibishana kunaleta mgawanyiko.”

GWAJIMA NA FLORA MBASHA
Februari 4,
mwaka huu picha za mtoto mchanga zilisambazwa katika mitandao ya kijamii
na kudaiwa kuwa ni wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha
aliyezaa na Mchungaji Gwajima.
Hatua hiyo ilikuja miezi kadhaa tangu Flora aingie katika mgogoro wa ndoa na mumewe Emmanuel Mbasha aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.
Akizungumza na MTANZANIA kuhusu taarifa za picha za mtoto huyo, Mchungaji Gwajima alisema ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora, Emmanuel Mbasha.
Mchungaji Gwajima alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo unaosambazwa dhidi yake kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora, anamwachia Mungu kila kitu.

“Si unajua hiyo
issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu… wakati mwingine mimi
huwa sijibu ujinga.“Awali niliwaza kuwashtaki (alipoanza kuhusishwa
kwamba ana uhusiano na Flora) wanaoeneza uzushi huo, lakini nikaona ‘It
doesn’t hold water’ (haina mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,”
alisema Mchungaji Gwajima.
tiko
tiko
Post a Comment