tiko
tiko
Rais
mstaafu Benjamin Mkapa amesema sekta ya uwekezaji nchini inashindwa
kukua kwa kasi inayotarajiwa kutokana na baadhi ya wanasiasa
kutokuielewa vizuri.
Akizungumza leo wakati wa kusaini
makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongea uwekezaji wa ndani na nje
nchini kati ya Taasisi inayoshughulikia mazingira ya uwekezaji Barani
Afrika (ICF) na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Mkapa ambaye pia ni
Mwenyekiti mwenza wa ICF alisema baadhi ya watu wanautazama uwekezaji
kama unyonyaji.
“Watu wanaona wanataka kunyonywa na sio kunyonyana,” alisema Mkapa wakati akielezea mafanikio ya TIC tangu kuanzishwa kwake.
Chini ya makubaliano hayo yaliyosainiwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa ICF, William Asiko na Mkurugenzi Mtendaji wa
TIC, Juliet Kairuki, ICF itakisaidia kituo cha uwekezaji nchini kukuza,
kuinua na kulingaza dirisha la uwekezaji na kuimarisha uwezo wake katika
kuwezesha na kufuatilia uwekezaji nchini.
Kairuku alisema Dola 950,000 (Sh1.7
bilioni) zitatolewa kwa ajili ya mradi wa dirisha la uwekezaji Tanzania
ambazo zitachangwa kwa pamoja kati ya ICF na Serikali ya Tanzania kwa
lengo la kurahisisha huduma zote zinazotolewa TIC kupatikana haraka, kwa
ufanisi na bila kupoteza muda.
“Huduma zote zinazotolewa na TIC sasa
zitakuwa zikipatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na kulipia ada
mbalimbali, tunajaribu kuwa wa kisasa,” alisema Kairuki na kuongeza kuwa
huduma hiyo itawanufaisha zaidi wawekezaji wa mikoani.
Mpango huo unatarajiwa kuwapa wananchi
nafasi ya kupata huduma zote za kituo hicho kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mapato nchini (TRA), Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya
HIfadhi za Jamii (SSRA) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(Brela) kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.
Mwenyekiti mwenza wa ICF, Neville Isdell
alisema uwekezaji unahitaji uwazi ili kuwavutia wafanyabiashara wa
ndani na nje kuendelea kuwekeza.
“Biashara zote hususani zilizo ndogo
zinahitaji kuwa na mazingira yaliyo mazuri watakayofanyia shughuli zao.
Kwa kuwa na dirisha la uwekezaji biashara nyingi zitaweza kukua,
kuongezeka na kushamiri haraka,” alisema Isdell.
Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji,
Christopher Chiza alisema mradi huo utakapokamilika utasaidia kuboresha
mazingira ya biashara na ushindani nchini.
“Kwa muda wa miaka michache iliyopita
nafasi ya Tanzania kimataifa katika kufanya biashara kwa mujibu wa
ripoti mbalimbali imekuwa hairidhirishi, ishara ambayo sio nzuri kwa
wawekezaji na sekta binafsi,” alisema Chiza.
tiko
tiko
Post a Comment