tiko
tiko
Mke wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere amesema kuwa mtoto wake, Makongoro Nyerere ana haki ya kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Ijumaa
wiki iliyopita, Makongoro alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi wake
kuhusu kuwania kiti hicho utajulikana mara kipenga kitakapopulizwa na
CCM.
Kauli
ya Makongoro ilitokana na uvumi uliokuwa umeenea katika mitandao ya
kijamii kuwa mtoto huyo wa tano wa mwalimu Nyerere alikuwa anaandaliwa
na watu waliofanya kazi karibu na mwalimu awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi ya habari nyumbani kwake Msasani jana, Mama Maria alisema mwanaye ana haki ya kugombea.
Mama
Maria aliyekuwa ameawaalika waandishi wa habari kuzungumzia uvumi
uliosambaa kuwa amefariki dunia, alitoa kauli hilo baada ya kuulizwa
kama uvumi huo unahusiana na habari kuwa mwanaye anataka kugombea urais.
Alisema,
“Hapana. Hayo mambo hayahusiani na mwanangu kutaka kuwania urais… yeye
ni raia wa Tanzania na hiyo ni haki yake ya msingi,”
Pia,
alidokeza kuwa wakati akizungumza na mwanaye mwingine juzi baada ya
uvumi wa kifo chake, naye alimwambia kuwa anataka kuwania nafasi hiyo.
Akitoa
ufafanuzi kuhusiana na uvumi huo alisema kuwa, taarifa za uvumi wa kifo
chake zilikuwa za furaha kwake na wala siyo za huzuni kama watu wengi
walivyodhania.
“Tumekuwa
tukifanya maombi ya kusali na kufunga kwa siku 40 kabla ya kipindi hiki
cha Kwaresima kwa ajili ya kuliombea taifa na dunia kwa ujumla. Na sasa
tunafunga tena, hivyo kwangu jambo hilo ni majibu ya maombi
tunayofanya. Nimefurahia kwa sababu naona maombi yanafanya kazi. Haya ni
majibu, tunasema tumepita mashetani,”alisema Mama Maria huku akitania
kuwa karne hii ni ya kisasa kweli, hata marehemu anaongea.
Aliongeza;
“Baada ya kupokea taarifa hizo, kwa kuwa nilikuwa nimelala nilichofanya
niliamka nikasali…nadhani Watanzania wanahitaji sana kusali, sala na
kazi. Kama Taifa pia tunahitaji kuwa na siku moja maalumu ya maombi.”
Licha
ya kusema kuwa taarifa hizo zilikuwa za furaha kwake, Mama Maria
alisema taarifa hizo zilizua hofu kubwa kwa familia yake na Taifa zima
kwa ujumla.
Alisema juzi mchana alianza kupokea simu kwa wingi tofauti na ilivyo kwa siku za kawaida.
Hata hivyo, alitoa angalizo kuwa huenda uvumi huo ukawa unahusiana na harakati za Uchaguzi Mkuu ujao.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko

Post a Comment