tiko
tiko
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika Febuari mwaka huu.
Historia
ya siasa duniani haitengani kwa kiwango kikubwa na historia ya dini.
Vitu hivi viwili kwa maisha ya mwanadamu vimekuwa sambamba na vyenye
mafanikio kwa jamii yoyote ile duniani. Kwa upande mwingine dini na
siasa vimeleta matatizo makubwa duniani.
Tusipojenga uhusiano mzuri kati ya siasa
na dini katika dunia na nchi yetu, tutaendelea kushuhudia machafuko na
uharibifu mkubwa wa mali pamoja na mauti dhidi ya binadamu kama
yalivyowahi kutokea hapa nchini hasa katika kampeni za kisiasa. Mara
nyingi maovu hayo yanasababishwa na uelewa mdogo juu ya uhusiano wa
siasa na dini.
Hivi sasa Tanzania imezalisha ugonjwa
mpya unaojulikana kwa jina la ‘udini.’ Unapoanza kuingiza udini katika
ajira, elimu, afya na siasa ujue kwamba usalama wa nchi upo hatarini.
Kutenganisha kabisa siasa na dini ni
kitu kisichowezekana katika dunia ya leo. Ndiyo maana ninaandika kwamba
“siasa bila dini ni uendawazimu”.
Uendawazimu
Huwezi kusema wewe unashughulika na
siasa halafu ukajidanganya kwamba huhusiki na masuala ya dini, wananchi
wengi ni waumini wa madhehebu mbalimbali. Mathalan, Tanzania kuna
Waislamu, Wakristo, Wabudha, Wahindu na hata wapagani.
Siasa ambayo haigusi maisha ya waumini
inakuwa imejitenga na jamii husika. Kitu muhimu na kinachotakiwa ni
kujenga uhusiano mzuri kati ya nyanja hizi mbili bila upotofu.
Katika siasa za Tanzania, nimegundua
kwamba kelele za muda mrefu zinazotolewa na Serikali na wanasiasa
kuwataka viongozi wa kiroho au wa dini wasichanganye dini na siasa
hazina msingi wowote ule kwa vile mambo hayo mawili
hayawezikutenganishwa kabisa.
Wanaoshikilia msimamo huo wanaonyesha woga wao juu na uelewa finyu katika masuala ya dini na siasa, hii ni bahati mbaya.
Yesu Kristo hakuhubiri habari za ufalme
wa Mungu pekee na kuacha dhambi, bali aligusa masuala ya jamii kama
amani, umaskini, kutenda haki, uhusiano mzuri, madhara ya rushwa na
ufisadi, wizi wa mali ya umma, utuanzaji wa rasilimali na hata kuponya
magonjwa. Na hii ndiyo injili sahihi, yaani injili ya jamii.
Yesu alikuwa akihubiri injili ya jamii,
je, sisi sasa hatupaswi kuihubiri injili hiyo? Nini msingi wa hofu ya
viongozi wa Serikali na wanasiasa kwa viongozi wa kiroho kuongelea
masuala ya kisiasa katika nyumba za ibada?
Kanisa Katoliki lilitoa msimamo wake
kuhusiana na kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa; Baraza la Maaskofu
Katoliki nchini Tanzania kupitia kwa Tume ya Haki na Amani kwa
ushirikiana na CPT, wametoa waraka au tamko ikipendekeza kusitishwa kwa
mchakato wa Kura ya Maoni ili kupisha maandalizi mazuri ya Uchaguzi
Mkuu. Je, hapo kanisa limefanya siasa?
-Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment