tiko
tiko
NYOTA wa
filamu za Kibongo Lungi Maulanga hivi karibuni anadaiwa kutupiwa jini
na wabaya wake wakiwemo wanafamilia yake kitendo kilichosababisha apooze
upande mmoja wa mwili wake.
Nyota wa filamu za Kibongo Lungi Maulanga.
Chanzo makini kinasema hofu yao kubwa ni
kuwa kitendo hicho kilifanywa na baadhi ya ndugu zake kufuatia tofauti
zao za kifamilia zilizosababisha kufikishana mahakamani.
“Katika shauri hilo mahakamani, yeye
alishinda, sasa baada ya siku mbili akaanguka na kupoteza fahamu,
alipozinduka akajikuta amepooza upande wa kulia, watu wanaunganisha
tukio hilo na kesi ya mahakamani,” kilisema chanzo.
Gazeti hili lilimkuta Lungi akiwa
amelala nyumbani kwake na alikiri kuanguka na kupooza na kwamba hawezi
kutembea vizuri lakini anamtumaini Mungu kuwa hali yake itakaa vizuri
kwani hana imani na mambo ya kishirikina.
tiko
tiko
Post a Comment