tiko
tiko
KWENU mastaa
wa Bongo Movies, bila shaka mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya
kila siku. Nawapongeza kwa hilo maana kazi nzuri tunaziona kila
kukicha.Mkitaka kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya, kama kawaida
naendeleza harakati zangu ndani ya mjengo wa Global Publishers.
Leo nimewakumbuka kupitia barua sababu
wengi wenu huwa hatupati muda wa kuzungumza. Naamini kwa barua hii
ujumbe utawafikia wengi kwa wakati mmoja.Dhumuni la barua hii ni kutaka
kuwakumbusha kuhusu suala zima la ugonjwa wa Ukimwi (Ngoma). Hakuna
asiyejua kwamba ugonjwa huu ni hatari na unaua.
Ndugu zangu, nimeguswa kuwaandikia barua
hii sababu ukweli ni kwamba aina ya maisha yenu wengi wenu nayajua.
Mara kwa mara tumekuwa tukisoma kuhusu nyinyi kushea mabwana na mabibi
kwenye magazeti yetu.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.
Kwa
nini msifanye kazi zenu za kuigiza ambazo zimewapa umaarufu. Sanaa si
ndiyo imewafanya muwe maarufu? Kwa nini mnaamua kuiweka kando?Hamtaki
kufanya kazi, mnataka kugombea mabwana wenye nazo. Mbaya zaidi mabwana
wenyewe mnaowagombea ndiyo walewale, fulani anamuona mwenzake anatembea
na mtu fulani basi na yeye anamzunguka kwa tamaa ya fedha.
, Nasibu Abdul ‘Diamond’Hata huyo
anayemzunguka mwenzake naye inafika wakati anapokonywa na mtu mwingine.
Katika mzunguko huo mmoja akiwa muathirika basi wote mmekwenda na maji.
Baadaye msururu wa mabwana unahamia
kwenda kwa mastaa wenzenu wa filamu, nao kila kukicha mnabadilishana.
Leo utasikia fulani anatembea na fulani kesho amehamia kwa
mwingine.Mastaa wa kiume wanatumia kigezo cha kudai watawachezesha
sinema wasanii wachanga, ngono zembe inatawala, hakuna tena kuwapa hata
hizo nafasi za kuigiza.
Jamani
katika ulimwengu huu wa sasa si wa zama zile. Watu wanapaswa
kubadilika, kuishi kisasa, kujitambua afya na kujikinga.Elimu imetolewa
ya kutosha, hakuna mtu asiyejua. Kwa nini muendelee kufanya ngono zembe
wakati mnatambua madhara yake? Kwa nini tunayahatarisha maisha yetu
kiasi hiki? Tubadilike!
Mastaa wa kike badilikeni, fanyeni kazi
msitegemee mabwana. Watanzania waliwajua kupitia sinema na michezo
ambayo mlikuwa mkiigiza, komaeni kupitia kazi hizo za sanaa muweze
kutengeneza kazi nzuri ambazo mtaziuza ndani na nje ya nchi.
Tumechoka kusikia habari za kukwapuliana mabwana. Tuseme inatosha kufanya ngono zembe.
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!
tiko
tiko
Post a Comment