tiko
tiko
SIKU za masikitiko bado zinaendelea kwa
waziri mkuu aliyejizulu, Edward Lowassa baada ya kuwepo kwa taarifa za
kukesha akilia, kisa kikitajwa kuwa ni mwendelezo ya maombolezo ya kifo
cha Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni John Komba.Kapteni Komba
alifariki dunia Februari 28, mwaka huu jijini Dar na kuzikwa kijijini
kwao, Lituhi mkoani Ruvuma, Machi 3.
Waziri mkuu aliyejizulu, Edward Lowassa.
Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka
kwa Lowassa kimefichua kuwa msiba huo ungali unamtesa waziri mkuu huyo
wa zamani kiasi cha kububujikwa na machozi kila mara na hasa nyakati za
usiku.
KIPI KINAMLIZA LOWASSA?
“Mfano juzi (Jumatatu, Machi 9) naambiwa hakulala, alikesha analia, inaonekana alimpenda kwa dhati (Komba), pengine ni kwa sababu alijitoa kumtetea, kumpigania na kumfariji kwenye mapambano yake ya kisiasa, tangu msiba huo utokee amekuwa kwenye wakati mgumu, siyo yeye peke yake hata mkewe (Regina Lowassa), wote wamefadhaika,” kilisema chanzo.

Uwazi Mizengwe lilipokidadisi chanzo
hicho kwa nini mheshimiwa huyo awe na wakati mgumu zaidi usiku, maelezo
yalikuwa ni kwamba, huo ndiyo wakati ambao Lowassa hupata muda wa
kupumzika na kutafakari maisha yake.
“Anapopata utulivu humkumbuka, mmoja
kati ya watoto wake aliniambia kuwa kauli za mzee wao mara kwa mara ni
kuona wanahuzunika naye pamoja ili hata wakipata fursa ya kufurahi,
wafurahi pamoja naye.
“Nafikiri unakumbuka Kapteni Komba
alitangaza hadharani kuwa anamuunga mkono Lowassa na yuko tayari hata
kufukuzwa chama, nadhani akikumbuka upiganaji wake na kuona amefariki
dunia anashindwa kuzuia huzuni, matokeo yake anabubujikwa machozi,”
kilisema chanzo hicho.
LOWASSA NA WARAKA WA KOMBA
Jumatano wiki hii, kupitia vyombo vya habari, Lowassa alisambaza waraka mzito wa kumlilia Kapteni Komba ambapo mbali na maneno mengine aliandika:“Hivi ni kweli sitasikia tena sauti yako Kapteni Komba! Mbona umeondoka bila kuniaga ndugu yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu.

“Kapteni Komba, mimi na wewe tumepigana
vita nyingi kwa maslahi ya chama na nchi yetu na kushinda vita hivyo.
Lakini bado tulikuwa tunaendelea na mapambano ya kumnasua Mtanzania
kutoka katika umaskini.”
MSAIDIZI WAKE ANENA
Wakati waraka huo ukiendelea kuwa gumzo kutokana na kuwagusa watu wengi, Uwazi Mizengwe liliwasiliana na msaidizi wa Lowassa, Abubakari Liongo ili kupata ufafanuzi wa taarifa za huzuni ya kiongozi wake inayomtokea mara kwa mara.

“Tunashukuru kwa sapoti tunayopata
kutoka kwa wananchi lakini kusema kweli mzee yuko kwenye wakati mgumu,
nafikiri ni kwa sababu anawapenda watu wake na asingependa kumpoteza
hata mmoja mpaka safari yake ya matumaini kwa Watanzania (hakufafanua)
itakapotimia.
WIMBO WA KOMBA KWA LOWASSA
Saa chache kabla ya kifo cha Kapteni Komba, habari zinaeleza kuwa mbunge huyo wa Mbinga Magharibi alimuandikia wimbo Lowassa wa kumsapoti kwenye mbio zake za urais akiamini kuwa waziri mkuu huyo wa zamani ndiye atakayeshinda kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuwa mgombea urais mwenye matumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

Wimbo huo ulikuwa na kiitikio:
“Jembe ni nani?
Huyu, huyu, huyu huyu anatufaa
Ni nani huyooo?
Huyu, huyu X3 Anatufaa
Jembe ni nani huyo?
Jembe ni Lowassa.
“Jembe ni nani?
Huyu, huyu, huyu huyu anatufaa
Ni nani huyooo?
Huyu, huyu X3 Anatufaa
Jembe ni nani huyo?
Jembe ni Lowassa.
Lowassa anatajwa kuwania urais mwaka huu
kuchukua mikoba ya mwanamtandao mwenzake, Rais Jakaya Kikwete ambaye
wakati anaingia ikulu alitajwa kuwa ni pacha wake kiasi cha wawili hao
kupewa jina la utani la Boys II Men, wakifananishwa na wasanii wa kundi
mahiri la muziki laini la nchini Marekani.
tiko
tiko
Post a Comment