tiko
tiko
KESI inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Ponda Issa Ponda, ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua ya utetezi haikuendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutofika mahakamani hapo jana.
Hakimu
Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo anayesikiliza kesi hiyo hakufika
mahakamani kwa kile kilichodaiwa mahakamani hapo kuwa amepatwa na
dharura, hivyo kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 2, mwaka huu.
Hakimu
Mfawidhi wa Wilaya ya Morogoro, Maua Hamduni ndiye aliyeahirisha kesi
hiyo baada ya mtuhumiwa na mawakili wa pande zote kufika mahakamani hapo
na kuarifiwa kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata dharura na
hivyo kushindwa kufika mahakamani.
Kwa
mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Morogoro, Shehe Ponda ataendelea
kukaa rumande hadi siku hiyo atakapoletwa tena mahakamani hapo.
Kesi
hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa mashtaka kujibu hoja zilizotolewa
na upande wa utetezi baada ya kufungwa kwa ushahidi ambazo zilidai kuwa
Shehe Ponda hakuwa na kesi ya kujibu.
Wakati
kesi hiyo inaahirishwa askari polisi wenye silaha, mbwa pamoja na
mabomu ya machozi waliendelea kuimarisha ulinzi katika eneo
linalozunguka mahakama hiyo.
Hata
hivyo, wafuasi wa Shehe Ponda walizuiwa kuingia ndani ya mahakama na
hivyo kubaki nje ya uzio wakiendelea kusoma Quran na kufanya maombi
licha ya mvua kunyesha.
Katika
kesi hiyo, upande wa mashitaka unaongozwa na mawakili wa Serikali,
Benard Kongola, Sunday Hyera na George Balasa, wakati upande wa utetezi
ukiwakilishwa na wakili Juma Nasoro na Abubakar Salimu.
Shehe
Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya
mahakama, kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu
kutenda kosa ambayo yote kwa pamoja anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka
2013 katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja cha ndege, Manispaa ya
Morogoro.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment