tiko
tiko
Hali
ya utoro kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano sasa imekithiri
baada ya ofisi ya chombo hicho cha kutunga sheria kusema kina taarifa za
wabunge 15 tu walioomba ruhusa kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Bunge hilo, linalotakiwa kuwa na wabunge
357, lilishindwa kupitisha miswada mitatu kutokana na upitishwaji wake
kuhitaji theluthi mbili ya wabunge wa kila upande wa Muungano.
Jana, wakati wa mjadala wa muswada wa
Sheria ya Usimamizi wa Maafa ambao uliwasilishwa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Jenister Mhagama
kulikuwa na idadi ya wabunge 81 tu bungeni, jambo linalomaanisha kuwa
takriban wabunge 250 hawakuwamo ndani ya chombo hicho cha kutunga
sheria.
Hali ilikuwa mbaya zaidi juzi. Wakati
kikao cha Bunge kikianza kujadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi na
Udhibiti wa Silaha na Risasi, kulikuwa na wabunge 29 tu ukumbini, hali
inayomaanisha kuwa zaidi ya wabunge 320 hawakumo ndani kujadili suala
hilo nyeti.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John
Joel aliiambia Mwananchi jana kuwa ni wabunge 15 tu ndiyo ambao wana
ruhusu ya Spika ya kutoshiriki kwenye vikao vinavyoendelea na kwamba
wengine wote wanapaswa kuwa bungeni.
“Wabunge 15 tu ndiyo wenye ruhusa,
wengine wapo lakini wanaingia na kutoka bungeni. Kutokuwepo kwao
kunaathiri sana wakati wa kupitisha miswada kutokana na kutotimia kwa
akidi.”
Idadi ya wabunge walio na ruhusa ni
ndogo sana kulinganisha na viti vingi vinavyokuwa vitupu wakati wa
mijadala mbalimbali kwenye vikao vya Mkutano wa 19 vinavyoendelea mjini
hapa, jambo ambalo ofisi ya Bunge imeleza kuwa inathiri shughuli
mbalimbali za Bunge zinazotakiwa kufanyika. Kwa mpangilio wa viti
bungeni, kawaida safu tatu tu za eneo moja huweza kuwa na viti zaidi ya
15.
Wawakilishi hao wa wananchi wanalipwa
Sh300,000 kwa siku, ikiwa ni fedha za posho ya kujikimu na vikao,
kiwango ambacho kwa kuzidisha kwa idadi ya wabunge 357 inafanya jumla ya
Sh107.1 milioni kutumika kwa siku moja.
Tangu kuanza kwa vikao vya Mkutano wa 19
wa Bunge Machi 17 mwaka huu hadi jana mchana, idadi ya wabunge imekuwa
ndogo ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika Mkutano wa 16 na 17 wa
Bunge uliokuwa na mahudhurio makubwa kutokana na kujadili sakata la
Akaunti ya Tegeta Escrow.
Katika mkutano wa 18 ulioisha Februari
mwaka huu wabunge wengi walikuwa wakichangia hoja, walijikita katika
kuzungumzia matatizo ya majimbo yao na kuacha mjadala uliokuwa mezani,
jambo ambalo lilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwataka wajikite
kwenye hoja za msingi na si kuzungumzia masuala ya majimbo yao.
Katika mkutano wa 19 unaoendelea hivi
sasa wabunge wamekuwa ni wachache, hali ambayo hulalamikiwa na baadhi ya
wabunge hasa ukifika muda wa kupitisha miswada mbalimbali.
Jana, kaimu kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kuwa utoro wa wabunge unakwamisha
mambo mengi ya msingi bungeni, huku akibainisha kuwa miswada haiwezi
kupitishwa huku kukiwa na idadi ndogo ya wabunge na kwamba kufanya hivyo
ni kukiuka kanuni.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment