tiko
tiko
AIBU! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na
tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji
Wastara Juma, Mark Edi.
Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye
maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha
uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini
alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.
“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka
elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua
kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha
Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili kuweza
kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai
amemchoka mwigizaji huyo.
“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini
kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati
hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye
kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.
Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa
matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada zinaendelea.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment