tiko
tiko
Kabuti Onyango si jina geni katika
tasnia ya filamu kama upon a mfuatiliaji wa mambo ya Bongo Movies
unamjua na unamkubali sana zaidi ya sana kama mpiga picha jongefu bora
Bongo bila shaka ana kitu muhimu na cha ziada ambacho ni muhimu sana.
Nakupa siri moja ambayo hauifahamu
kuhusu Kabuti, ni mtoto wa mwigizaji mahiri wa filamu na vichekesho Mzee
Joseph Onyango ambaye toka ameanza kuigiza hajawahi kupoteza uwezo wake
wa kuigiza katika kiwango cha ubora katika tasnia.
Tofauti ya Kabuti na wasanii wengine
mara nyingi japo hawezi kuigiza ulazimisha kurithi vipaji vya wazazi wao
badala ya kufanya kitu ambacho wanamudu na kuwa mahiri zaidi, kwa
Kabuti hilo alilibaini na kugundua kuwa uwezo wake ni kamera na
anaikung’uka kweli.
Ana kitu cha ziada mtaalum huyu ana
uwezo kuitangaza kazi yake anayoifanya na kuwafikia watu wote kwa
wakati, mfano mzuri ni pale msanii huyu alipokuwa akifanya kazi na Salma
Jabu ‘Nisha’ sote tulijua sinema ya Nisha iliyokuwa sokoni ijayo na
iliyopita.
Baada ya kutengana na msanii huyo Kabuti
aliingia makubaliano na mwanadada jembe mtayarishaji makini wa filamu
Jennifer Kyaka aka Odama kufungua mlango tu kaingia na kitu cha Jada
kila mtu kakubali kuwa Kabuti ni zaidi ya Camerman kwa kifupi jamaa
ANAJUA.
tiko
tiko
Post a Comment