tiko
tiko
Jeshi
la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata silaha aina ya SMG yenye
risasi 29 pamoja na mabomu matatu ikiwa ni sehemu ya silaha mbili
walizoporwa askari Polisi waliokuwa doria mwezi januari mwaka huu ambazo
walinyang'anywa na vikundi vya uhalifu ambavyo vilikuwa vimeweka kambi
maalum katika eneo la mleni maji moto lililopo amboni jijini Tanga.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoani Tanga Bwana Juma Ndaki amesema mtuhumiwa
aliyekutwa na silaha hiyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za
kiupelelezi alikamatwa katika eneo la kabuku lililopo barabara kuu ya
Chalinze -Segera ndipo alipobanwa na kukiri kuwa yeye na kundi lake
wameficha silaha yenye namba 14303545 katika mapango ya amboni iliyokuwa
ikikutumika katika operesheni iliyokuwa ikifanywa na vikundi vya
uhalifu.
Katika
hatua nyingine ya kukabiliana na makundi ya uhalifu kutoka ndani na nje
ya nchi, idara ya uhamiaji wilayani Lushoto imewaaagiza wananchi kutoa
taarifa kwa mamlaka husika endapo wataona baadhi ya wageni kutoka nchi
jirani ya Kenya wakiingia nchini kupitia njia za panya kufuatia baadhi
ya wageni kudaiwa kupitisha silaha na kuingia nazo nchini kinyume cha
sheria.
Kufuatia
hatua hiyo mkuu wa wilaya ya Lushoto Bibi Mariam Juma ambaye yeye na
kamati yake ya ulinzi na usalama alikuwa akigawa hati za kusafiria kwa
watu watano waliopewa na idara ya uhamiaji amewagiza viongozi wa
serikali kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao na akawataka
waliopewa hati za kusafiria kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa
kufuatia baadhi ya watanzania kujiingiza katika vitendo vya usafirishaji
wa dawa za kulevya.
tiko
tiko
Post a Comment