tiko
tiko
MWAKA mmoja
uliopita nilikutana na mwanasiasa kijana January Yusuf Makamba na
kumuuliza kama ana wazo la kugombea urais; jibu lake lilikuwa ni: “Ni
wazo sahihi.”
Sikumwelewa alimaanisha nini, lakini
habari zilizopo mtaani hivi sasa kuwa anakusudia kuchukua fomu za kuomba
uteuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye kuingia kwenye
kinyang’anyiro cha kugombea urais nimeelewa kuwa jibu lake wakati ule
lilimaanisha; NDIYO.
Ni wazi mtu kuamka na wazo la aina hii,
kwamba na mimi nataka kugombea urais, ukimsikia akisema hivyo lazima nia
yake hiyo itakuwa na historia. Bila shaka January amewaza jambo hilo
tangu zamani, pengine kwa sababu amelelewa kwenye mikono ya mwanasiasa
ambaye ni baba yake au amenogewa na uhondo wa uongozi.
JANUARY MAKAMBA NI NANI?
Ni mwanasiasa kijana aliyezaliwa Januari 28, 1974. Ameishi katika kijiji cha Mahenzagulu wilayani Lushoto, mkoani Tanga. Amesoma Shule ya Msingi Handeni, akaingia Sekondari ya Galanos na Forest Hill.
Baadaye alitimkia nchini Marekani ambako alisoma kozi fupi zinazohusu masuala ya amani kabla ya kuingia Chuo Kikuu cha George Mason alikochukua Masta yake katika Sayansi kuhusu Uchambuzi na Ufumbuzi wa Migogoro.

Alipohitimu masomo yake Makamba ambaye
mama yake mzazi anaitwa Josephine mwenyeji wa Missenyi mkoani Kagera,
alirejea nchini na kuajiriwa kama mtumishi daraja la pili katika Wizara
ya Mambo ya Nje ambayo kwa wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Rais Jakaya
Kikwete.
ALIANZAJE SIASA?
Pamoja na kwamba January amelelewa na mwanasiasa Yusuf Makamba aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, kijana huyo hakuwa amechipuka kwenye anga hizo hadi pale alipojiunga rasmi kwenye mtandao uliokuwa ukiratibu harakati za Rais Kikwete kuingia madarakani.

Akiwa na umri mdogo, January alitumika
vilivyo kwenye mtandao huo, akisafiri sehemu mbalimbali kushawishi
makundi ya watu wamuunge mkono bosi wake wakati huo ili ashike dola,
jambo ambalo liliwezekana mwaka 2005.
Baada ya Mheshimiwa Kikwete kuingia
madarakani, hakuifukia lulu ya January pengine kwa sababu aliona umahiri
wake wakati wa harakati. Rais hakujali umri mdogo aliokuwa nao kijana
huyo, alimsogeza ikulu na kumfanya kuwa msaidizi wake akisimamia kazi
maalum za kiongozi huyo wa nchi.
Utumishi wa nafasi hiyo ulizidi kumjenga
mwanasiasa huyo, ingawa hakutajwa sana kwenye vyombo vya habari, lakini
mgogoro wa dili la ‘Malaria No More’ wa mwaka 2008, ulioibuka kati yake
na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, ulimleta kwenye sura ya
jamii na kuonekana yupo na pengine watu walipata fursa ya kumperuzi kwa
lengo la kumjua zaidi.
January alimudu nafasi ya usaidizi wa
rais kwa miaka mitano mfululizo, mwaka 2010 aliamua kutema utamu wa
ikulu na kwenda kugombea ubunge katika jimbo la Bumbuli mkoani Tanga
ambako alishinda kwa kishindo na kuthibitisha uwezo wake kisiasa.
MAISHA YA UBUNGE NA UWAZIRI
Baada ya kuingia bungeni 2010, January alianza kuwa mwiba mchungu kwa serikali, michango yake makini kwenye mijadala ya bunge iliwavutia wananchi wengi. Fumba na kufumbua aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ambapo aliiongoza vizuri.

Moja kati ya matunda aliyotoa mbunge
huyo kwenye kamati yake ni pale alipoonesha ujasiri wa kukabiliana na
wizara ya nishati katika tatizo la mgao mkali wa umeme lililokuwa
likiitesa nchi wakati huo. Msimamo wake ulikuwa ni kutafuta suluhu ya
tatizo hata ikiwezekana baadhi ya maslahi ya wafanyabiashara na viongozi
wa serikali kuguswa.
Mwaka 2012 January alichaguliwa kuwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, huku nyota ya mwanasiasa huyo kijana
ikiendelea kung’aa kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano
Sayansi na Teknolojia
ANAFAA KUINGIA IKULU
Sifa za kuingia ikulu anazo, hakika ni kijana aliyejipambanua kupitia utumishi wake kwa jamii kuwa ni mtu makini, mbunifu na mwenye dira ya maendeleo na uwezo wa kuleta mabadiliko kwenye mazingira magumu.

Katika nafasi ndogo aliyopewa ya unaibu
waziri, kiongozi huyo ameonesha kwa vitendo kupambana na ufisadi ndani
ya shirika la simu (TTCL) huku akibuni mikakati ya namna ya kulifufua
na kulifanya liondokane na kasumba ya kujiendesha kwa ubia.
January ni mtu wa vitendo, mfuatiliaji
wa mambo, muumini wa haki na msimamizi wa mali za umma. Kabla ya kuwa
mbunge aliandika kitabu alichokiita ‘Bumbuli Jana, Leo na Kesho’ ambacho
kilichambua matatizo ya jimbo hilo na namna ya kuyashughulikia.
Mpaka leo mwanga wa maendeleo katika
jimbo hilo umeanza kuonekana, hii inamaanisha kwamba kiongozi huyo
kijana ambaye ameandika pia kitabu cha ‘Tanzania Mpya’ ni hazina
isiyotakiwa kupotezwa kwa namna yoyote.
Katika masuala ya siasa na hasa
unapozungumzia sifa za mgombea lazima awe anauzika na mwenye mvuto
kwenye jamii, vitu ambavyo January kwa jinsi alivyo, ameonesha kuwa
navyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amemuelezea January kuwa ni kijana makini.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amemuelezea January kuwa ni kijana makini.
CHANGAMOTO ZAKE
Pamoja na sifa alizonazo mbunge huyo kijana bado kuna changamoto nyingi ambazo zinaweza kukwaza safari yake ya kwenda ikulu, miongoni mwa hizo ni kukosa mtandao. Mbali na ndani ya chama chake hata nje nako January haonekani kama ana watu wengi wanaomuunga mkono katika safari yake ya urais. Ushindi wa kisiasa unahitaji mtaji wa watu, usipokuwa nao wa kutosha matarajio yako ya kushinda yanakuwa hafifu mno.

Changamoto nyingine ninayoiona kwa
January ni kuhukumiwa kwa makosa ya baba yake. Ripoti ya uchunguzi wa
mdororo wa CCM iliyowakilishwa na Wilson Makama mwaka 2011, ilionesha
kwamba katibu mkuu wakati huo, Yusuf Makamba, alikuwa dhaifu kwenye
kusimamia baadhi ya mambo.
Mbali na hilo taarifa za chini kwa chini
ndani ya CCM zinaeleza kwamba mzee Mkamba alikuwa na msuguano na baadhi
ya viongozi na makada nguli wa chama.
Kwa tabia za Kiafrika ni rahisi sana
udhaifu wa baba kuhukumiwa nao mtoto na maadui wa wazazi kuwa wa familia
nzima, tafsiri ambayo inaweza kumuondolea uungwaji mkono January na
hasa ndani ya chama chake.
Hata hivyo, mtazamo huu unaweza kuwa siyo wa kudumu endapo juhudi za kumaliza dosari zikichukuliwa.
Hata hivyo, mtazamo huu unaweza kuwa siyo wa kudumu endapo juhudi za kumaliza dosari zikichukuliwa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment