tiko
tiko
Staa na mrembo kutoka Bongo Movies,
Irene Uwoya, amewataka wasanii chipukizi wenye ndoto ya kuigiza naye
katika filamu yake mpya wawasiliane naye ili awajumuishe katika filamu
hiyo.
Uwoya alitoa fursa hiyo kupitia ukurasa
wake wa Instagram ambapo alisema, anafanya hivyo ili kunyanyua wasanii
chipukizi wanaokosa nafasi za kuigiza na mastaa licha ya kuwa na uwezo
mkubwa wa uigizaji.
“Najiandaa kwa ajili ya kazi yangu mpya
na natumaini itakuwa nzuri kwani hatua niliyofikia ni kutoa nafasi kwa
chipukizi kushiriki filamu hiyo kwa kuwa ni jambo la busara,” alieleza
Irene.
Irene ambaye amejijengea umaarufu mkubwa
kupitia filamu yake ya ‘Oprah’, aliyoigiza na Kanumba ambaye ni
marehemu kwa sasa, ametamba kuendelea kuibua vipaji vipya zaidi vya
wasanii wa filamu.
tiko
tiko
Post a Comment