tiko
tiko
Serikali imeagiza wakuu wote wa mikoa, kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wote waliofaulu mitihani ya darasa la saba, wanajiunga na shule za sekondari katika kipindi hiki kabla ya Machi 28 mwaka huu, vinginevyo watakaokwamisha watoto hao watachukuliwa hatua kali.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri MkuuTawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Kasimu Majaliwa
katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora (RCC), kilichoketi
katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini hapa juzi.
Alisema
kila mkoa unatakiwa kujiwekea mkakati wa kuhakikisha watoto wote,
waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za
sekondari wanaripoti ili wasipoteze fursa hii muhimu waliyopata kwa
kisingizio cha namna yoyote ile iwe wazazi au vinginevyo.
‘Ili
zoezi hili liende vizuri na watoto wote waripoti kwa asilimia 100,
suala la usimamizi ni la muhimu sana na kila halmashauri inapaswa
kutekeleza wajibu wake ipasavyo, vinginevyo mtakuwa mnakwamisha malengo
ya serikali ya kufanikisha mpango wa matokeo makubwa sasa’, aliongeza.
Aliagiza
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote,
kuhakikisha kila mzazi au mlezi atakayehusika kwa namna moja au nyingine
kukwamisha au kuzuia mtoto wake kujiunga shule ya sekondari,
anachukuliwa hatua kali mara moja ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment