tiko
tiko
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (Necta) Dk. Charles Msonde.
Hatua za
kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya waliohusika katika udanganyifu wa
mitihani ya kidato cha nne wa mwaka 2014 ambao wanafunzi 184 wamefutiwa
matokeo kutokana na udanganyifu huo.
Kati ya
wanafunzi waliofutiwa matokeo 128 ni wa kujitegemea kutoka vituo viwili
vya P2617 Kisesa mkoani Mwanza na P4806 Ubago Visiwani Zanzibar na 56 ni
watahiniwa kutoka shule mbalimbali.
Akitangaza
matokeo juzi jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani
Taifa (Necta) Dk. Charles Msonde, alisema wameiagiza mamlaka husika
kuwachukulia hatua za kinidhamu waliohusika katika vituo hivyo kwa
mujibu wa kanuni za utumishi.
“Lazma wahusika
wachukuliwe hatua kwani udanganyifu uliojitokeza ni karatasi moja ya
kujibia mtihani kuandikwa na watu watatu tofauti, jambo linaloonyesha
hakukuwa na umakini,” alisema
Katika matokeo
hayo wanafunzi 196,805 (68.33%) wamefaulu kati ya watahiniwa wote
288,247 waliofanya mtihani huo huku kiwango cha ufaulu kikipanda kwa
asilimia 10.08 ikilingnishwa wanafunzi 235,22 wailofaulu mwaka 2013
(58.25%).
Hata hivyo,
kiwango hicho cha ufaulu bado hakijafikia dhamira ya Serikali ya lengo
la Matokeo Makubwa Sasa (BRN) la kufikia aslimia 70, jambo linalohitaji
nguvu zaidi kwa walimu, wanafunzi na wadau wote wa elimu.
Dk. Msonde
alisema matokeo ya mwaka huu yanaonyesha bado ufaulu wa masomo mengi upo
chini ya aslimia 50, Hisabati (19.58), Biashara (34.29), Historia
(37.41), Jiografia (37.96), Uraia (37.90), Fizikia (46.71) na Kutunza
Fedha (42.20).
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment