tiko
tiko
KWA
mara nyingine, nchi imejikuta katika aibu nyingine ya mauaji ya kutisha
dhidi ya mtoto mdogo mwenye ulemavu wa ngozi, wanaojulikana kama
Albino, Yohana Bahati (1) siyo pichani yaliyotokea huko Geita hivi
karibuni.
Huu ni mwendelezo wa mauaji ya jamii hii ya watu, ambao kwa miaka mingi
sasa, wanasadikika kuwa chanzo cha unafuu wa maisha kwa baadhi yetu.Yapo
madai kwamba baadhi ya viungo vya Albino, vinawapa utajiri au nafasi za
kisiasa kwa wanaohitaji, ndiyo maana wako tayari kuondoa uhai wa wenzao
ili kiu yao itimie. Siyo walemavu wa ngozi tu, bali kuna mauaji pia ya
ndugu zetu wanaotafutwa kwa ajili ya viungo vyao vingine na mambo haya
yametokea kwa miaka mingi sasa.
Vyombo vyetu vya usalama vinafahamu kuhusu uhalifu huu, lakini kwa namna
ya kusikitisha, vimeshindwa kuukomesha, licha ya ukweli kwamba uko
ndani ya uwezo wake. Jeshi letu la Polisi, ambacho ni chombo chenye
intelijensia ya hali ya juu, haliwezi kuwa halijapata dawa ya kulitibu
tatizo hili, ambalo hutokea kwa namna ileile, kwa watu walewale na mara
nyingi, katika maeneo yaleyale.
Tunajua kuwa uhalifu huu unaandamana na imani za kishirikina na kwa
maana hiyo, wahusika wakubwa walio mstari wa mbele ni hawa wanaojiita
waganga wa jadi. Kama jeshi letu lingekuwa na nia thabiti ya kudhibiti
genge hili la mauaji, bila shaka lingeanza na kundi hili ambalo
lingewaongoza kuwapata matajiri na wanasiasa wanaotajwa kunufaika na
mauaji haya.
Ni vipi Jeshi la Polisi kwa miaka yote limeshindwa kukomesha mauaji haya
yanayotokea katika mikoa ya kanda ya ziwa pekee? Maana kila siku
tunasikia kuhusu Albino kuuawa au kukatwa viungo vyao katika M ikoa ya
Mwanza, Geita, Simiyu, Shinganya na maeneo ya jirani.
Kama kwa miaka yote tumeshindwa kuwabaini waganga feki wanaodanganya
watu, pamoja na wale wanaotumika kuua, basi hakuna jinsi ambavyo
hatuwezi kuacha kuhisi kuweko kwa ushirika wenye shaka baina ya watu
walio katika mamlaka na wauaji hawa.
Na hawa wenye mamlaka ndiyo wanaolifanya jambo hili lionekane la
kawaida, ambalo linashughulikiwa kikawaida, jambo ambalo ni lazima
tupige kelele za hapana kwa nguvu kubwa!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment