tiko
tiko
Kibano! Jamaa mmoja ambaye jina
halikupatikana mara moja, amejikuta akinusa kifo baada ya kula kipigo
‘hevi’ wakati akifanya jaribio la wizi wa fedha kiasi cha shilingi laki
450,000 kupitia huduma za fedha kwa mitandao ya simu.
Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa
Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kijitonyama jijini Dar
ambapo jamaa huyo alidaiwa kuingia kwenye duka moja akijifanya anataka
kutoa shilingi laki nne na nusu (450,000/=) jambo lililomfanya wakala
kumuonesha namba za kutolea kwa uchangamfu akijua ni mteja wa kawaida.
Dakika chache baadaye wakati wateja
wengine wakiendelea kuhudumiwa, jamaa huyo alionesha meseji kuwa ametoa
kiasi hicho cha fedha kupitia moja ya mitandao ya simu.
Wakala huyo alipoichukua meseji ya jamaa
huyo ili kuhakikisha muamala wake alishangaa kuona meseji hiyo kuwa ni
ya mtandao mwingine tofauti na alioutaja huku ikionesha imeandikwa au
kutumwa na namba ya kawaida ya simu badala ya namba ya huduma hiyo ya
mtandao husika.
Wakizidi kumshushia kichapo.
Wakala huyo, Maulid Vedasto alishangaa
na kuamua kumshikilia jamaa huyo akimuitia mwizi ndipo wananchi wenye
hasira kali walipofika na kumzingira wakimtaka atoe maelezo ya kutosha
ambapo njemba huyo ilikiri kutaka kuiba jambo lililoamsha hasira za watu
walioamua kumshushia kipigo hevi nusura afe.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wakala
huyo alisema kuwa jamaa huyo alifika mara ya kwanza siku hiyo dukani
kwake akitaka kutoa shilingi elfu sabini lakini alighairi na kurudi
baada ya muda mfupi akitaka kufanya jaribio hilo la wizi.
Kichapo kikiendelea.
“Nilianza kumtilia shaka mara ya kwanza
alipokuja na kujifanya anataka kutoa fedha huku akiwa na wasiwasi na
kila mara alipokuwa akiwaona watu wengi ndipo alipokuwa akiniongelesha
akijifanya ana haraka ya kutoa fedha, akiona watu wachache anasubiri,”
alisema wakala huyo.Baada ya kunaswa jamaa huyo alipekuliwa kwenye simu
yake ambapo iligundulika kuwa kweli meseji hiyo haikuwa ya mtandao
husika huku akiwa hana salio.
Katika kuhakikisha hilo, wakala huyo
aliwapigia simu makao makuu ya mtandao huo na kupata taarifa kuwa hakuna
salio la aina hiyo lililohamishwa kutoka kwenye simu ya jamaa
huyo.Katika utetezi wake, jamaa huyo aliomba watu wasimuue kwa kuwa ni
tamaa za kidunia zilimponza huku akikiri kufanya utapeli huo kwa
kushirikiana na wenzake watatu ambapo wamefanikiwa kutapeli mawakala
kibao jijini Dar.
“Jamani
inatosha mlivyonipiga, naomba msiniue ni shetani tu amenipitia. Kweli
nakiri kuwa nimewaibia mawakala wengi sana lakini nimekoma. Nipelekeni
polisi msiniue,” alisema jamaa huyo ambaye alikuwa akivuja damu
chapachapa kisha kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’
kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment