Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

BWANA HARUSI APATWA NA UCHIZI SHEREHE IKIENDELEA

tiko tiko
KAMA kawa, kama dawa. Ni siku nyingine mapaparazi wetu wanaotii amri za mkuu wao, Musa Mateja ‘Toz’, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba au Mzee wa Mji Kasoro Bahari’, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ na Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana na Mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga- Mwenge, jijini Dar.
Saa 3:14 usiku
Banana Zoro akitumbuiza.
BWANA HARUSI APATWA NA UCHIZI SHEREHE IKIENDELEA
Mkuu akiwa ofisini anamaliza kunywa supu ya utumbo, anafuta mustachi, anabonyeza kizenji batani za simu yake ya kisasa na kumtwangia Mkude Simba.
Shekidele: Naam Mkuu wangu nakupata sawia, huku Moro hatujambo vipi habari za Dar, jiji la maraha?
Makao Makuu: Shekidele acha mbwembwe nieleze uko pande zipi muda huu?
Shekidele: Mkuu niko nje ya Ukumbi wa Kings Way, Msamvu kuna tukio la bwana harusi kupatwa na uchizi wakati sherehe ya harusi ikiendelea.
Makao Makuu: Mweeh, ilikuwaje?
Shekidele: Mkuu nasikia sherehe ilianza salama lakini ilipofikia wakati wa zawadi ndipo bwana harusi akachanganyikiwa na kuanza kuvua suti na kutaka kubaki mtupu lakini wageni waalikwa wakamuwahi.
Makao Makuu: Dah! Huyo mke aliyemuoa ni mke wa mtu nini?
Shekidele: Mkuu hilo sina uhakika nalo lakini muda huu ndiyo naongea na baba wa bwana harusi aliyejitambulisha kwa jina la Omary Milomo.
Makao Makuu: Anasemaje Milomo?
Shekidele: Hata yeye anasema hajui chanzo lakini nasikia kuna ndugu wamemkimbiza kwa mganga wa kienyeji kufanya utafiti na kupewa tiba.Makao Makuu: Dah! Kweli Moro ya leo si mchezo, haya Shekidele piga kazi mimi ngoja nimcheki Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos. Saa 5:56 usiku
VIGOGO WANASWA WAKICHANGAMKIA MACHANGU
Bukos: Naam mkuu wangu nakupata sawia.
Makao Makuu: Haraka eleza uko wapi?
Bukos: Mkuu wangu nimetoka Mikocheni Club East 24 kwenye onesho la B Band.
Makao Makuu: Sawa, muda huu upo wapi?
Bukos: Nimepita hapa Ukumbi wa Cheetoz, Kijitonyama ambapo usiku huu ilibidi wakamue Mashujaa Musica lakini hawapo.
Makao Makuu: Sasa uko wapi?
Bukos: Mkuu niko hapa Barabara ya Shekilango eneo la Ambiance, Sinza naangalia magari ya serikali yanavyozoa machangudoa, kuna kundi la machangu liliizunguka Bajaj lakini baada ya kutokea Land Cruiser mbili zenye namba za serikali wale machangu wamemtelekeza yule mteja aliyeletwa na Bajaj wameyakimbilia ma Cluiser.
 Saa 6:34 usiku
MKUU ACHIMBA MKWARA
Makao Makuu: Mkuu anapiga simu ya Mateja inaita zaidi ya mara sita bila kupokelewa hatimaye inapokelewa na Mateja akiwa kwenye usingizi wa pono.
Mateja: Mmmh… oyaaa nani wee unatusumbua usiku wote watu tumelala?
Makao Makuu: Shaaaabashiiii… we Mateja unasemajeee…?
Mateja: Dah! Chondechonde Mkuu wangu sikujua kama naongea na wewe, nisamehe sana bosi wangu.
Makao Makuu: Shukuru Mungu umeniomba msamaha ungejuta kunifahamu.
 Mateja: Nashukuru mkuu.Makao Makuu: ngoja nimcheki Issa Mnally Mzee wa GX 100.
Saa 7:23 usiku
MZEE WA GX 100 AENDA KUWAFUNGIA KAZI WAFANYA MAOVU WA MWANZA
Mnally: Ha…ha…halooo m… mm… Mkuu habari za Makao Makuu?
Makao Makuu: Hapa ni salama kabisa vipi uko wapi muda huu?
Mnally: Mkuu niko Nzega.
Makao Makuu: Sawasawa Mzee wa GX 100 ukifika Mwanza wewe kama Kamanda wa OFM natumai ndani ya muda mfupi utasafisha uovu wote wa jiji hilo. Sasa tunataka kuona mafumanizi ya Jiji la Mwanza siyo kila siku Dar.
Mnally: Ondoa shaka Mkuu, yatakuwa yakumwaga.   

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top