tiko
tiko
China na Sheria zao, Serikali ya nchi
hii ni moja kati ya chache ambazo zimekuwa mstari wa mbele kwenye
utekelezaji wa chochote kile ambacho watakiamua, kwa wakati wowote na
kwa njia yoyote.
Moja ya stori za mwisho mwisho kusikika
kutoka China ni ishu ya kila mtu kutakiwa kujisajili kwenye mitandao ya
kijamii kwa majina yote halali yani, yale ambayo yanatambulika kwenye
cheti cha kuzaliwa au passport hivi.
Kuna hii nyingine ya kuhusu hiyo hiyo
mitandao, unaambiwa Mamlaka ya Mawasiliano China wamefuta website 65
ambazo watu walizitumia kwa masuala ya mapenzi ikiwemo kutafuta wapenzi
na kushare picha za ngono.
Mitandao hiyo iligundulika kwamba watu walikuwa wakijisajili kwa majina fake, halafu wanashare picha, video za ngono pia.
Rungu limeanza kazi ndani ya China,
yeyote anayetaka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii lazima ajisajili
kwa jina lake kamili, hii itakuwaje mfano ikianza Bongo kwa kasi hii hii
mtu wangu!
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment