tiko
tiko
Mfumuko wa bei kwakwa mwezi januari umeshuka hadi kufikia asilimia 4.0
kutoka asilimia 4.8 ya Desemba mwaka jana kutokana na kupungua kwa bei
za bidhaa mbalimbali ikielezwa kwamba kupungua huko kulikuwa hakujatokea
kwa miaka miwili iliyopita.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo
alieleza kuwa kushuka huko kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandaji
bei ya bidhaa na huduma ikilinganishwa na ilivyokuwa Desemba .
Amesema mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji umepungua hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.7 ya mwezi Desemba.
Ametaja baadhi ya vyakula vilivyochangia kushusha mfumuko huo kuwa ni
mahindi yaliyoshuka kwa asilimia mahindi 13.3, unga wa mahindi (6.2),
samaki (2), ndizi za kupika (11.3), mihogo (12.0)
Kwa mujibu wa Kwezigabo bidhaa zisizo za chakula nazo zilipungua. Mafuta
ya taa yalishuka kwa asilimia 8.4, dizeli (10.2), petroli (6.8) na gesi
ya kupikia ilishuka kwa asilimia 2.9. Takwimu hizo mpya zinaonyesha
kuwa fahirisi za bei zimeongezeka kutoka 146.0 Januari 2014 , hadi
kufikia 152.43 Januari mwaka huu.
“Bidhaa zisizo za vyakula kama vile mavazi ya wanawake,mkaa na kodi nazo
zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa fahirisi katika mwezi
huu”amesema Kwezigabo
Amefafanua kuwa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi hadi mwezi
umeongezeka kwa asilimia 2.0 ikilinganishwa na ongezeko la 0.2 Desemba
mwaka jana.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment