tiko
tiko
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limeahidi kuwa limejipanga vizuri, kukabiliana na vurugu na matukio ya kihuni kuelekea uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Mihayo Msikhela alipozungumza na mwandishi ofisini kwake mjini hapa jana.
“Hatutakuwa
na msalie Mtume kwa mtu yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani na
kufanya mambo ya kihuni wakati wa uchaguzi, tunataka kila mmoja apate
nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani kuanzia kampeni hadi
siku ya kupiga kura,” alisema Kamanda Mihayo.
Kamanda
Mihayo alisema wanaendelea kujiandaa kikamilifu, kuhakikisha uchaguzi
wa mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu mkubwa ili kutoa nafasi kwa
kila mwananchi kushiriki vema kumchagua kiongozi anayemtaka.
“Tutakomesha waleta vurugu,” alisema.
Alisema uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa wenye ushindani na changamoto
mbalimbali, ambazo zinahitaji wadau wote kushirikiana kuhakikisha kuwa
suala la amani na utulivu linapewa nafasi kubwa.
Alisema
polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama,
wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na
hawako tayari kuona kuna baadhi ya watu wachache wanauvuruga.
Alisema
kila mmoja ahakikishe anadumisha utulivu uliopo. Alisema ni vizuri kwa
watu wote, wakiwemo wagombea na wafuasi wao, kuheshimu sheria zilizopo
na kujiepusha na mambo yatakayowafanya washindwe kutimiza ndoto zao za
kuwa viongozi au kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Alisema
kuna baadhi ya watu wamekuwa na fikra potofu, kudhani kwamba kipindi
cha uchaguzi ndicho muda wa mwafaka wa kuvunja sheria.
Alisisitiza
kuwa moja ya mambo watakayokuwa nayo makini katika uchaguzi wa mwaka
huu ni kuwadhibiti watu hao, bila kujali chama cha siasa cha mhusika.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment