tiko
tiko
Hii
ni hali ya mkusanyiko wa maji kuzunguka kifuko cha mayai. Ni ngozi
laini na nyepesi juu ya kifuko cha mayai. Kifuko cha mayai huwa
kinachipua vifuko vidogovidogo ‘Follicles’ na endapo follicles hizi
zitakuwa na ukubwa zaidi ya sentimeta mbili, basi ndiyo huitwa Ovarian
Cyst. Uvimbe unaweza kuwa na ukubwa kuanzia saizi ya punje ya njegere
hadi saizi ya ukubwa wa chungwa.
Aina nyingi ya uvimbe huu huwa hauumi na hauwi saratani na huweza
kutokea na kupotea ingawa unaweza kuwa mkubwa zaidi. Ovarian Cyst
huwatokea wanawake wa umri wote kuanzia watoto wachanga hadi mwanamke
anapofikisha umri wa kuzaa. Uvimbe pia hutokea hata kwa wanawake
waliokoma hedhi. Baadhi ya aina hizi za uvimbe huleta matatizo mfano
kuvuja damu na maumivu makali au kugeuka kuwa kansa.
Endapo uvimbe utakuwa mkubwa zaidi ya sentimeta tano, basi upasuaji
utafanyika kuuondoa lakini ukiwa chini ya hapo unaweza kutibika kwa
dawa. Aina za uvimbe wa Ovarian Cyst Uvimbe huu unaweza kutokea
kufuatana na mzunguko wa hedhi na huitwa ‘functional cyst’ ambapo huu wa
‘Ovarian Cyst’ unaweza kuwa mkubwa endapo utakuwa na zaidi ya sentimeta
tano na kuwa mkubwa zaidi hadi kufikia ukubwa hadi usawa wa kitovu.
Uvimbe ambao hutokea wakati wa hedhi kitaalamu huitwa functional cyst na
umegawanyika kwenye makundi matatu ambayo ni ‘Follicular Cyst, Corpus
Luteum Cyst na Thecal Cyst’.
Aina hizi za uvimbe huwa hazizidi ukubwa wa sentimeta tatu na wastani hukaa kwa kati ya siku tano hadi tisa na hupotea wenyewe.
Aina hizi za uvimbe huwa hazizidi ukubwa wa sentimeta tatu na wastani hukaa kwa kati ya siku tano hadi tisa na hupotea wenyewe.
Aina hizi zinatokea kufuatana na mfumo wa hedhi uitwao ‘Functional’ na
uvimbe ambao hutokea bila ya uhusiano na hedhi huitwa ‘Non Functional’
ambao kwa vyovyote huhitaji uchunguzi wa kina.
DALILI
Dalili za uvimbe unaowatokea watoto wadogo wa kike kabla ya kuvunja ungo huitwa Juvenile Ovarian Cyst na umegawanyika katika makundi tofauti. Kama tulivyosema huwa mkubwa hadi kufikia usawa wa kitovu na kumsababishia mtoto alalamike kuumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara.

Maumivu haya huwa makali hata kabla uvimbe haujawa mkubwa. Maumivu pia
humpata hata mwanamke mwenye uvimbe ambaye tayari ameshakuwa au
ameshavunja ungo.Hapa mwanamke hulalamika maumivu ya mara kwa mara ya
tumbo chini ya kitovu na hushika hadi kiuno na maumivu wakati wa tendo
la ndoa.
Mtoto mdogo wa kike mwenye uvimbe pamoja na kulalamika maumivu, pia
hupata tatizo la kutokwa na mkojo mara kwa mara na kukojoa kitandani,
hata kufunga kupata haja kubwa.
Uvimbe huu husababisha mwanamke avurugikiwe na mzunguko wa hedhi, apate
maumivu kabla ya hedhi au maumivu makali wakati wa hedhi na damu kutoka
kwa muda mrefu na kidogokidogo.
Huhisi tumbo limejaa, zito au hata tumbo kuvimba upande mmoja au lote. Inaweza kutokea uvimbe ukapasuka wenyewe tumboni na kumsababishia maumivu makali sana ya ghafla chini ya kitovu upande wa kulia au kushoto.

Mgonjwa kushindwa kumaliza kutoa mkojo hasa uvimbe unapokuwa mkubwa,
yaani ukikojoa mkojo hauishi au unapata haja kubwa haiishi na unajikuta
unakaa sana chooni. Mwanamke anayesumbuliwa na uvimbe pia hulalamika
maumivu ya kichwa, mwili kuchoka mara mwa mara, kichefuchefu na kutapika
pamoja na kuhisi uzito unaongezeka.
Dalili nyingine hutegemea na aina za uvimbe, mfano mwanamke mwenye
tatizo la vivimbe vidogovidogo vingi katika vifuko vya mayai huanza
kuona ongezeko la vinyweleo mwilini, mkononi, miguuni na hata masharafu
usoni, kutokea kwa chunusi nyingi usoni na mgongoni.
Kuwa mnene sana na kitambi na ugumba yaani hupati ujauzito kwa muda
mrefu endapo chanzo cha tatizo ni hitilafu katika tabaka la ndani la
kizazi. Uchunguzi Tatizo hili la uvimbe
Uchunguzi hufanyika katika hospitali kubwa za rufaa ambapo vipimo vya
Ultrasound vitafanyika na ikibidi hata CT- Scan itafanyika. Kipimo cha
damu kuangalia mfumo wa homoni au vichocheo kitafanyika. Vipimo vingine
vitategemea hali ya mgonjwa kwa kipindi hicho kwa jinsi daktari
atakavyoona inafaa kufuatana na dalili alizonazo mgonjwa.
TIBA
Matibabu na ushauri Matibabu hutolewa baada ya uchunguzi wa kina ambapo utapewa dawa za kutuliza maumivu na nyingine ambazo daktari ataona zinafaa. Uvimbe mkubwa tiba yake inaweza kuwa dawa au upasuaji kutegemea na uvimbe pia kama kuna tatizo la kutopata ujauzito matibabu yatafanyika sambamba na kutibu uvimbe.

Ni vema kwenda hospitali, muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa
kina. Tatizo hili huchunguzwa kisayansi zaidi ili kuepuka madhara
yatokanayo na uvimbe huo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment