Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MCHAKATO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA SASA KUIVAA

tiko tiko

Mchakato wa mpango wa serikali wa kuhamia Dodoma umefikia katika hatua ya kupata maoni ya sekretarieti ya baraza la mawaziri.
Hayo yamesemwa bungeni mjini Dodoma Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mh Agrey Mwanry wakati akijibu swali la mbunge wa chilonwa mh Hezekiah Chibulunje aliyetaka kufahamu sababu za serikali kushindwa kupeleka bungeni muswada wa sheria kusudiwa huku ikiendelea na ujenzi wa majengo ya wizara na taasisi za serikali katika jiji la Da es salaam.
Ameongeza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2010/2011 serikali tayari imetoa agizo la kuzuia ujenzi wa majengo mapya ya wizara katika jiji la Dar es salaam.
Amesema serikali itaweka utaratibu mahususi kupitia kanuni zinazotungwa na waziri mwenye dhamana ya ustawishaji makao makuu kwa lengo la kuharakisha na kuwezesha utekelezaji wa sheria ikiwemo ukomo wa muda ambao serikali itahamia makao makuu ya nchi.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top