tiko
tiko
SIKU chache
baada ya kuvuja kwa picha zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul
‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo
kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond,
Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio
hilo.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.

Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo
hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili
isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa
mwaka jana.
“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo
Zari azidi kumganda Diamond, asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili
mambo mengine yaendelee kwa sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu
haukuwa na baraka zangu,” alisema mama Wema.
Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayehiheshimu kwa sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume
gani amuoe lakini nahitaji mtu mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe
ndio anaweza kuwa baba wa familia la sivyo inakuwa ni mambo ya
kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa Diamond.”
Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli
hiyo ya mama Wema, simu yake iliita bila kupokelewa lakini kupitia
ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia
picha ya Zari huku akizungushia duara tumboni na kuandika; ‘kileee
kinaanza kumharibia mtu mavazi.’
tiko
tiko
Post a Comment