tiko
tiko
STAA wa
muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya aina yake
baada ya kusema anavutiwa na taasisi huru ya imani ya Freemason kutokana
na umakini mkubwa walionao kwenye kazi zao. Akipiga stori na paparazi
wetu, Baby alisema watu wengi wamekuwa wakizungumza kwa mitazamo tofauti
kuhusiana na Freemason lakini kiuhalisia, watu wa imani hiyo ni makini
wanaojitambua na kujiheshimu.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
“Hawa jamaa kiukweli siyo wa kuchezewa
kabisa, lakini ukweli tu ni kwamba nawazimikia mno na ndiyo sababu mara
nyingi hata ukiangalia kazi zangu za muziki utakutana na nembo zao
kivyovyote vile, sema siwezi kujiunga nao,” alisema Baby Madaha.
tiko
tiko
Post a Comment