tiko
tiko
Kamishna Kova akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)
Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)
KAMISHNA wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman Kova leo ametoa tamko
mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama cha Wananchi
CUF (JUVICUF) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika hapo kesho.
Kamanda Kova amewataka vijana wa CUF kutoandamana kesho na kama
wataandamana jeshi hilo halitakuwa tayari kuona maandamano hayo
yakifanyika .
Alisema kuwa maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kesho
Februari 13 mwaka huu kutoka Buguruni, Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja,
Mtaa wa Ohio hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kisha Wizara ya Mambo ya
Ndani ,kwa dhumuni la kuitaka Tume ya Taifa ya Uchanguzi (NEC) iongeze
siku za uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutoka siku
saba hadi siku 14, pamoja na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu
unaofanywa na jeshi la polisi nchini.
Kova ametaja sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa siku waliyoomba ni
siku ya kazi, ambapo maandamano hayo yakifanyika yatasumbua mfumo mzima
wa shughuli za jiji zima, kibiashara, huduma za afya, walemavu, watoto
na n.k.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment