Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

BINTI WA MIAKA 27 AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA.. WIVU WA KIMAPENZI WAHUSISHWA -SHINYANGA VIJIJINI

tiko tiko
Mwili wa Marehemu Huma ukiwa unachukuliwa na Maafisa wa Polisi

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia juzi.

Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa.

Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokua amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa.

Wananchi wa Kata Solwa wakiutazama Mwili wa Marehemu eneo la Tukio

Mwili wa Marehemu Huma Simon ukiwa eneo la tukio

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top