Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

ATM, Supermarket, Internet.. Hizi zote unaambiwa ndani ya Magereza China !!

tiko tiko
PAY-Inmates-rehab
Movie ya Shawshank Redemption ni moja ya movies ambazo story yake inahuzunisha, jamaa anakamatwa na kufungwa gerezani kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake lakini kosa hilo hakulifanya yeye.
Gerezani akampata rafiki ambaye ni mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha muda mrefu, alikuwa akimsaidia kwa vitu vingi, baadaye jamaa akaachiliwa huru, alipofika mtaani alijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na mabadiliko makubwa ambayo aliyakuta.
Sasa ili kuepusha mazingira magumu kwa wafungwa baada ya kumaliza vifungo vyao, Beijing wametengeneza mji mdogo ndani ya gereza kwa ajili ya wafungwa waliohukumiwa kifungo cha muda mrefu, miji hiyo ina huduma kama ATM, treni za umeme, huduma za Benki, hii ni kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao kuona namna mambo yanavyoenda uraiani.
Huduma nyingine zilizoko ndani ya magereza hayo ni pamoja na Internet Cafe na supermarkets.
Sababu ya Serikali kuamua hivyo ni kuwepo kwa matukio ya watu wengi kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutumikia vifungo ya muda mrefu na kukuta uraiani vitu vingi vimebadilika kutokana na mabadiliko ya maendeleo ambayo huwa yanatokea kila wakati.
the-shawshank-redemption-poster-2Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top