tiko
tiko
Waziri wa Usalama nchini Kenya Joseph
Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa
gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa
kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.
Bwana Nkaissery amempa mnyakuzi wa ardhi
hiyo siku moja kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi
kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.
Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.
(CHANZO: BBC SWAHILI)
tiko
tiko
Post a Comment