tiko
tiko
Wengi
wanaifahamu Mikumi kama hifadhi ya taifa ya wanyama iliyopo mkoani
Morogoro. Lakini pia Mikumi ni jimbo la uchaguzi lililopo ndani ya
Wilaya ya Kilosa, likiwa na ukubwa wa karibu kilometa 7,353.
Wiki iliyopita, kama kawaida Gazeti la
Uwazi lilichanja mbuga mpaka kwenye jimbo hilo linaloongozwa na
mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amer kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) ambaye pia ndiye mmiliki wa kampuni ya SAS na kuzungumza na
wananchi mbalimbali ambao walieleza matatizo yanayowakabili jimboni
humo.
MATATIZO YA WANANCHI NA MAJIBU YA MBUNGE
Naftali Kigoda, mkazi wa Kijiji cha Lumango, alikuwa na haya ya kusema: “Sisi wananchi tunaoishi pembeni ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi tunanyanyasika sana kwa kweli.
Naftali Kigoda, mkazi wa Kijiji cha Lumango, alikuwa na haya ya kusema: “Sisi wananchi tunaoishi pembeni ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi tunanyanyasika sana kwa kweli.
“Ukilima kashamba kako, wanyama wanatoka
kwenye hifadhi na kuja kula na kuharibu kila kitu. Pia maisha yetu yapo
hatarini kwa sababu simba wakishikwa na njaa, wanakuja huku vijijini na
kusababisha madhara makubwa kwa binadamu na mifugo yetu, tunaomba
mheshimiwa mbunge atusaidie.
Prudencia Safari, mkazi wa Kijiji cha
Msindazi, naye alieleza tatizo hilohilo la wanyama wakali na waharibifu
kuvamia katika makazi ya watu na kusababisha madhara makubwa, ikiwemo
vifo vya wanakijiji wanaoliwa na wanyama wakali kama simba.
Wilfred Akyoo, mfanyabiashara katika Mji
Mdogo wa Mikumi, yeye alikuwa na haya ya kusema: “Tatizo kubwa Mikumi
ni uzembe wa viongozi wetu. Hawawajibiki ipasavyo kutimiza ahadi
wanazotoa wala kutuondolea matatizo yanayotukabili. Maji ni shida, dawa
hospitali ndiyo hakuna kabisa lakini wao wapo tu. Halafu viongozi wetu
hawana utaratibu wa kuitisha mikutano na kutusomea mapato na matumizi.”
“Michango imezidi shuleni, yaani kila
mara watoto wanasumbuliwa kisa michango. Tunaomba mheshimiwa mbunge
atusaidie. Kingine kuna rushwa sana polisi, yaani mtu ukikamatwa hata
kama huna kosa hutoki bila kutoa rushwa, hii siyo sawa kabisa,” Emanuel
Chedieli aliliambia Uwazi.
Tatizo lingine ambalo Uwazi
lililishuhudia, ni mabinti wengi wadogo kukatisha masomo na kujihusisha
na biashara haramu ya kuuza miili yao, kwa madereva wa malori
yanayotumia barabara kuu ya Iringa- Morogoro ambapo vitendo hivyo
vinafanyika waziwazi bila kificho.
“Ukosefu wa ajira ni tatizo huku kwetu,
vijana wengi tunashinda tu vijiweni kama hivi, hakuna kazi wala huwezi
kupata mtaji wa kufanya biashara ya maana. Tunaomba mbunge wetu
atusaidie,” Malick Mgunda aliliambia Uwazi.
“Mimi namwambia mheshimiwa mbunge asikie
kilio chetu sisi wananchi wa Msolwa, tunahangaika sana na hili tatizo
la ardhi ambalo yeye anahusika kwa kupewa ardhi yetu ya kilimo kufanyia
kazi za makampuni yake. Tunaomba asikie kilio chetu atuachie ardhi
tuendelee na kilimo mbona eneo ni kubwa sana?” mwananchi ambaye hakutaka
jina lake liandikwe gazetini aliliambia Uwazi.
MAELEZO YA MBUNGE
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mheshimiwa mbunge Abdulsalaam Seleman Amer ambaye alikiri kuzijua kero mbalimbali za wananchi wa jimbo lake na kueleza jinsi anavyohangaika kuzipatia ufumbuzi.
Kuhusu suala la wananchi na mali zao kudhuriwa na wanyama, mbunge huyo alisema amekuwa akihangaika kwa kipindi kirefu kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kujenga uzio wa kuzuia wanyama kuingia kwenye makazi ya watu wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana na hifadhi.
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mheshimiwa mbunge Abdulsalaam Seleman Amer ambaye alikiri kuzijua kero mbalimbali za wananchi wa jimbo lake na kueleza jinsi anavyohangaika kuzipatia ufumbuzi.
Kuhusu suala la wananchi na mali zao kudhuriwa na wanyama, mbunge huyo alisema amekuwa akihangaika kwa kipindi kirefu kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kujenga uzio wa kuzuia wanyama kuingia kwenye makazi ya watu wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana na hifadhi.
Kuhusu michango ya watoto shuleni,
mbunge huyo amewataka wananchi kutokuwa wazito katika kuchangia
maendeleo yao au ya watoto wao kwa sababu serikali peke yake haiwezi
kufanya kila kitu kwa wakati kutokana na kuchelewa kwa bajeti kuu.
Suala la ardhi anayomiliki kwenye Kijiji
cha Msolwa, mbunge huyo alisema eneo hilo analimiliki kisheria na
kwamba hakuna mtu yeyote aliyeonewa, akaongeza kuwa hata hivyo
majadiliano yanaendelea kati yake na wananchi na anaamini watafikia
muafaka mzuri.
tiko
tiko
Post a Comment