tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Mwili wa marehemu Daudi Lusalula Mbatiro(56) baada ya kuchinjwa Desemba 5,2014-Picha kutoka maktaba ya malunde1 blog
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kunasa mtandao wa watu
wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya watu kwa kuchinja kwa
visu,ikiwemo tukio la mauaji ya Katibu wa
Chama Chama Mapinduzi kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Daudi Lusalula Mbatiro(56) aliyeuawa kwa kuchinjwa kama kuku mwaka jana
kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa
Tukio la kuuawa kwa katibu huyo wa CCM lilitokea Desemba 5,2014 saa
mbili usiku wakati katibu huyo wa CCM kata ya Mwaluguru ambaye pia
alikuwa ni katibu wa elimu,malezi na mazingira baraza la wazazi wa CCM
wilaya ya Kahama akitokea kata ya Kagongwa kwenda nyumbani kwake
Sungamile baada ya kutoka kwenye mkutano wa chama chake uliokuwa
unafanyika mjini Kahama.
Waliotajwa
na jeshi la polisi kuhusika katika mtandao huo ni pamoja na diwani wa
kata ya Mwalugulu wilayani Kahama Bundala Kadilanha(CCM),mfanyabiashara
wa Kagongwa Tobo Mwanasana,pamoja na Emmanuel Maziku,Masanja
Shepa,Samwel Seni Budugu na Shija Shepa.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus
Kamugisha alisema katika uchunguzi wa mauaji ya katibu wa CCM kata ya
Mwalugulu Daudi Mbatiro jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa Emmanuel
Maziku na Masanja Shepa na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na
mauaji hayo.
Alisema
baada ya kuwahoji watuhumiwa hao wawili,waliwataja wahusika wengine
ambao ni Bundala Kadilanha(diwani wa Mwalugulu),Tobo
Mwanasana(mfanyabiashara,Samweli Seni Budugu mkazi wa Mwakitolyo na
Shija Shepa mkazi wa Mwalumba Kahama.
Alisema
awali jeshi la polisi baada ya kupata taarifa za watu hao liliweka
mtego kwa kuwapigia simu ili kuwakodi kufanya mauaji katika kijiji cha
Nyindu na kufanikisha kuwakamata watu hao ambao hujihusisha na matukio
mbalimbali ya mauaji.
Alisema
baada ya kuwafanyia mahojiano watu hao wawili walikiri kuhusika na
matukio ya mauaji katika mkoa wa Shinyanga na Tabora kwa kukodiwa ili
kuchinja watu kwa kisu na wao sio wakata mapanga ingawa wanaua vikongwe
na kulipiza kisasi.
Kamanda
Kamugisha alisema watuhumiwa walisema kiongozi wao ni Samweli Seni
Budugu na wenzake ni Tobo Mwanasana,Bundala Kadila na Shija Shepa na
kabla ya mauaji hayo wanaenda kupakwa dawa kwa waganga wao wa jadi ambao
ni John Shija mkazi wa kijiji cha Lyabukande na mwingine aliyetajwa kwa
jina moja la Tabu mkazi wa Kizungu.
Kamanda
Kamugisha alisema watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na matukio ya
mauaji ya marehemu Ngolo Sakumi(69) mkazi wa Mwalugulu na walikodiwa kwa
shilingi 1,000,000/= aliyewakodi ni Jikuba Kajile na Lukuba Nangi.
Tukio
jingine walilokiri kuhusika ni mauaji ya Mary Seleman Masenya(45) mkazi
wa kijiji cha Matinje na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= na wanawake
watatu ambao ni wake wenza wa marehemu.
Alitaja
tuko jingine walilohusika ni lile la mauaji ya Mboje Seni(70) mkazi wa
kijiji cha Butondo na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= walikodiwa na
Mwanabundi mkazi wa Butondo na tukio jingine ni mauaji ya Kwigema
Lubinza(60) mkazi wa kijiji cha Kakulu kata ya Nyahanga.
Kamanda
huyo alisem jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwakamata wahusika
wengine wa matukio hayo ikiwa ni pamoja na waganga wa kienyeji
waliohusika huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia
kukamatwa kwa wahusika wote wa mauaji ya kukodiwa na mauaji ya vikongwe
ili kukomesha kabisa mauaji hayo.
BOFYA HAPA KUSOMA HABARI YA KUCHINJWA KWA KATIBU HUYO WA CCM ILIYORIPOTIWA NA DUNIA KIGANJANI
tiko
tiko
Post a Comment