tiko
tiko
Dawa
zinazotajwa kufutiwa usajiri na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na
dawa za kutibu maralia ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine, dawa za
kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsulis zenye kiambata cha
Fenil Propanolamine nyingine ni dawa ya sindano aina ya Chrolaphenical
inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India, dawa za kutibu
fungus ya vidinge na kapsuli.
Akitangaza
dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Bw. Hiit
Sillo hatua hiyo imefikiwa baada ya uchuguzi wa kitaalam wa muda mrefu
kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia
unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa
shirika la afya duniani WHO.
Aidha
TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP kutumika
kama kinga ya maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza
watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo
mkurugenzi wa dawa TFDA Bw. Mitanga Fimbo pamoja na kufafanua athari
anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza
mara moja kabla ya kuanza kwa msako.
tiko
tiko
Post a Comment