tiko
tiko
Nisiku nyingine nzuri ya Ijumaa
tunapokutana kwenye zulia zuri la mahaba, tukijuzana, kubadilishana
mawazo na kuelimishana mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.
Ni matumaini yangu kwamba kwa uwezo wa
Mungu uko poa kabisa, leo nataka tujadiliane kuhusu mada hii nyeti na
muhimu kama inavyojieleza; hakuna adhabu nyingine ya kumpa mwenzi wako
anapokukosea zaidi ya kumkatalia kuwa naye faragha?
Nimesukumwa kuandika mada hii baada ya
kupokea ujumbe kutoka kwa msomaji wangu aliyeomba hifadhi ya jina lake,
ambaye alikuwa akilalamika kwamba kwa muda mrefu, mkewe amekuwa na
kawaida ya kutumia tendo la ndoa kama silaha yake anapokosewa na mwenzi
wake.
Kwamba ukimkosea hata kwa jambo dogo,
basi anaweza kununa hata mwezi mzima na katika kipindi chote anachonuna,
hataki kumpa haki yake ya ndoa mpaka atakapoamua mwenyewe.
Akaendelea kunieleza kwamba kutokana na
tabia hiyo, amefikia hatua ya kutafuta mchepuko ambao huwa unamliwaza
kipindi mkewe anapoamua kumuadhibu kwa kumnyima haki yake ya ndoa.
Huyu ni mmoja kati ya wanaume wengi
ambao wamegeuka kuwa wahanga wa ndoa zao wenyewe, kwa wenzi wao kukataa
kuwa nao faragha inapotokea wamegombana au kupishana kauli ndani ya
nyumba.
Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara, mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine na huwezi kuwa bora katika mahusiano kama hujifunzi mambo mapya na kuyaelewa kwa kina.
Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara, mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine na huwezi kuwa bora katika mahusiano kama hujifunzi mambo mapya na kuyaelewa kwa kina.
Katika utafiti mwepesi nilioufanya,
nimegundua kuwa hata wanawake wa zamani, walikuwa wakitumia silaha hii
ili kuwaweka sawa wenzi wao na kuwafanya waone umuhimu wa kuwa na mke.
Kwamba
kama mwanaume amefanya kosa ambalo limemkasirisha mwanamke na hana
namna nyingine ya kumfikishia ujumbe, basi njia nyepesi ni kukataa kuwa
naye faragha. Kwa sababu wanaume wengi wana udhaifu katika suala hili,
inakuwa rahisi kwao kushuka chini, kuzungumza kwa upole na unyenyekevu
ili kutafuta suluhu na hatimaye mambo yaendelee kuwa mazuri kama
ilivyokuwa mwanzo. Kama nitakuwa nimekosea, wanawake watu wazima mnaweza
kunirekebisha kwa manufaa ya wasomaji wangu.
Hata hivyo, hali imekuwa tofauti kwa
wanawake wa kizazi cha sasa ambapo hawaitumii silaha hiyo inavyotakiwa,
badala yake wanaona ndiyo njia nyepesi ya kuwakomoa wenzi wao na siyo
njia ya kufikisha tena ujumbe kama walivyokuwa wakifanya wanawake wa
zamani.
Matokeo yake, wanaume nao kwa sababu
wanaona wanaonewa, wanaamua kutafuta njia mbadala; kwamba kwa sababu
wewe umeamua kumkomoa mwenzi wako kwa kukataa kuwa naye faragha kwa muda
mrefu mpaka utakapoamua mwenyewe, naye anatafuta wa pembeni wa kumpoza
mtima wake.
Mkirudi ndani, kila mmoja analala mzungu
wa nne, wakati wewe ukifikiri umemkomoa kwa ‘kumlaza njaa’, mwenzako
anatumia muda mrefu kutafakari mapenzi aliyopewa na mchepuko wake.
Taratibu anaanza kuhamisha mapenzi kutoka kwako kwenda kwa mwizi wako na
mwisho ananogewa.
Muda ambao wewe unataka suluhu, yeye
tayari ameshazama kwenye dimbwi la mahaba ya mchepuko. Kutakuwa na ndoa
tena hapo? Kutakuwa na amani tena hapo? Akili za kuambiwa changanya na
zako.
Watafiti wa saikolojia ya mapenzi, wanaeleza kwamba hakuna njia inayoweza kuwaunganisha wawili wapendanao, hata kama walikuwa wamegombana kiasi gani, kama tendo la ndoa linalofanyika kwa ukamilifu.
Watafiti wa saikolojia ya mapenzi, wanaeleza kwamba hakuna njia inayoweza kuwaunganisha wawili wapendanao, hata kama walikuwa wamegombana kiasi gani, kama tendo la ndoa linalofanyika kwa ukamilifu.
Wewe unasemaje kuhusu hili? Ni sawa
kumbania mwenzako kwa kipindi kirefu kwa sababu tu amekuudhi? Kuwa huru
kutuma mawazo yako kupitia namba zilizopo hapo juu. Tukutane wiki ijayo
tutakapoendelea kuijadili mada hii. Tchao!
tiko
tiko
Post a Comment